Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Mwanzo 26:14 - Swahili Revised Union Version

14 Akawa na mali ya kondoo, na mali ya ng'ombe, na watumwa wengi. Hao Wafilisti wakamhusudu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 Alikuwa na makundi ya kondoo, ng'ombe na watumwa wengi, hata Wafilisti wakamwonea wivu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

14 Alikuwa na makundi ya kondoo, ng'ombe na watumwa wengi, hata Wafilisti wakamwonea wivu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 Alikuwa na makundi ya kondoo, ng'ombe na watumwa wengi, hata Wafilisti wakamwonea wivu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 Akawa na mifugo ya kondoo na ng’ombe, na watumishi wengi sana, kiasi kwamba Wafilisti wakamwonea wivu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 Akawa na mifugo ya kondoo na ng’ombe, na watumishi wengi sana, kiasi kwamba Wafilisti wakamwonea wivu.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

14 Akawa na mali ya kondoo, na mali ya ng'ombe, na watumwa wengi. Hao Wafilisti wakamhusudu.

Tazama sura Nakili




Mwanzo 26:14
16 Marejeleo ya Msalaba  

Naye akamtendea Abramu mema kwa ajili yake; naye alikuwa na kondoo na ng'ombe, na punda dume, na watumwa, na wajakazi, na punda majike, na ngamia.


Naye Abramu alikuwa tajiri sana kwa mifugo, kwa fedha, na kwa dhahabu.


na BWANA amembarikia sana bwana wangu, amekuwa mtu mkuu; amempa kondoo, na ng'ombe, na fedha, na dhahabu, na watumishi, na wajakazi, na ngamia, na punda.


Abrahamu akampa Isaka yote aliyokuwa nayo.


Kwa hiyo mtu huyo akazidi mno, akawa na wanyama wengi, na vijakazi, na watumwa, na ngamia, na punda.


Ndugu zake wakamhusudu; bali baba yake akalihifadhi neno hili.


Mali yake nayo ilikuwa ni kondoo elfu saba, na ngamia elfu tatu, na jozi za ng'ombe mia tano, na punda wake mia tano, na watumishi wengi sana; basi hivi mtu huyo alikuwa ni mkuu sana kuliko watu wote wa upande wa mashariki.


Basi hivyo BWANA akaubariki huo mwisho wa Ayubu zaidi ya mwanzo wake; naye alikuwa na kondoo elfu kumi na nne, na ngamia elfu sita, na jozi za ng'ombe elfu moja, na punda wake elfu moja.


Kwani hasira humwua mtu mpumbavu, Nao wivu humwua mjinga.


Asiye haki ataona na kusikitika, Atasaga meno yake na kuondoka, Matumaini ya wasio haki hupotea.


Nyumbani mwake mna utajiri na mali, Na haki yake yadumu milele.


Baraka ya BWANA hutajirisha, Wala hachanganyi huzuni nayo.


Ghadhabu ni kali, na hasira ni gharika; Lakini ni nani awezaye kusimama mbele ya wivu.


Tena nikagundua kuwa juhudi zote, na ustadi wote katika kazi, hutokana na mtu kumwonea mwingine wivu. Hayo nayo ni ubatili na kufukuza upepo.


Sauli akamwonea Daudi wivu tangu siku ile.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo