Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Mwanzo 18:10 - Swahili Revised Union Version

10 Akamwambia, Hakika nitakurudia wakati huu huu mwakani, na tazama, Sara mkeo atapata mwana wa kiume. Sara akasikia mlangoni pa hema iliyokuwapo nyuma yake.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

10 Mmoja wao akasema, “Hakika nitakurudia wakati kama huu mwakani, na mkeo Sara atakuwa na mtoto wa kiume.” Sara alikuwa huko nyuma mlangoni mwa hema, akisikiliza.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

10 Mmoja wao akasema, “Hakika nitakurudia wakati kama huu mwakani, na mkeo Sara atakuwa na mtoto wa kiume.” Sara alikuwa huko nyuma mlangoni mwa hema, akisikiliza.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

10 Mmoja wao akasema, “Hakika nitakurudia wakati kama huu mwakani, na mkeo Sara atakuwa na mtoto wa kiume.” Sara alikuwa huko nyuma mlangoni mwa hema, akisikiliza.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

10 Kisha Mwenyezi Mungu akasema, “Hakika nitakurudia majira kama haya mwaka ujao, na Sara mkeo atakuwa na mwana.” Sara alikuwa akiwasikiliza kwenye ingilio la hema lililokuwa nyuma ya Ibrahimu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

10 Kisha bwana akasema, “Hakika nitakurudia tena majira kama haya mwakani na Sara mkeo atakuwa ana mwana.” Sara alikuwa akiwasikiliza kwenye ingilio la hema, lililokuwa nyuma yake.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

10 Akamwambia, Hakika nitakurudia wakati huu huu mwakani, na tazama, Sara mkeo atapata mwana wa kiume. Sara akasikia mlangoni pa hema iliyokuwapo nyuma yake.

Tazama sura Nakili

Mwanzo 18:10
15 Marejeleo ya Msalaba  

Malaika wa BWANA akamwambia, Hakika nitauzidisha uzao wako, wala hautahesabika kwa jinsi utakavyokuwa mwingi.

Nami nitambariki, na tena nitakupa mwana kwake, naam, nitambariki, naye atakuwa mama wa mataifa, na wafalme wa makabila ya watu watatoka kwake.

Mungu akasema, Sivyo, lakini Sara mkeo atakuzalia mwana wa kiume, nawe utamwita jina lake Isaka. Nami nitafanya agano langu imara kwake kuwa agano la milele kwa ajili ya uzao wake baada yake.

Bali agano langu nitalifanya imara kwa Isaka, ambaye Sara atakuzalia majira kama haya mwaka ujao.

Wakamwambia, Yu wapi Sara mkeo? Akasema, Yumo hemani.

BWANA akamjia Sara kama alivyonena, na BWANA akamfanyia kama alivyosema.

Sara akapata mimba akamzalia Abrahamu mwana wa kiume katika uzee wake, kwa muhula alioambiwa na Mungu.

Lakini yule malaika akamwambia, Usiogope, Zakaria, maana dua yako imesikiwa, na mkeo Elisabeti atakuzalia mtoto wa kiume, na jina lake utamwita Yohana.

Lakini yule wa mjakazi alizaliwa kwa mwili, yule wa mwanamke huru kwa ahadi.

Basi, ndugu zangu, kama Isaka sisi tu watoto wa ahadi.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo