Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Mathayo 23:9 - Swahili Revised Union Version

9 Wala msimwite mtu baba duniani; maana Baba yenu ni mmoja, aliye wa mbinguni.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 Wala msimwite mtu yeyote ‘Baba’ hapa duniani, maana Baba yenu ni mmoja tu, aliye mbinguni.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

9 Wala msimwite mtu yeyote ‘Baba’ hapa duniani, maana Baba yenu ni mmoja tu, aliye mbinguni.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 Wala msimwite mtu yeyote ‘Baba’ hapa duniani, maana Baba yenu ni mmoja tu, aliye mbinguni.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 Nanyi msimwite mtu yeyote ‘Baba,’ hapa duniani, kwa maana mnaye Baba mmoja, naye yuko mbinguni.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

9 Nanyi msimwite mtu yeyote ‘Baba’ hapa duniani, kwa maana mnaye Baba mmoja, naye yuko mbinguni.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

9 Wala msimwite mtu baba duniani; maana Baba yenu ni mmoja, aliye wa mbinguni.

Tazama sura Nakili




Mathayo 23:9
16 Marejeleo ya Msalaba  

Basi Elisha alikuwa ameshikwa na ugonjwa wake uliomwua; naye Yehoashi mfalme wa Israeli akateremka amtazame, akamlilia mbele yake, akasema, Baba yangu! Baba yangu! Gari la Israeli na wapanda farasi wake!


Naye Elisha akaona, akalia, Baba yangu, baba yangu, gari la Israeli na wapanda farasi wake! Asimwone tena kabisa; akashika mavazi yake mwenyewe, akayararua vipande viwili.


Naye mfalme wa Israeli alipowaona, akamwambia Elisha, Ee baba yangu, niwapige? Niwapige?


Mwana humheshimu baba yake, na mtumishi humcha bwana wake; basi, kama mimi ni baba yenu, heshima yangu iko wapi? Na kama mimi ni bwana wenu, kicho changu ki wapi? BWANA wa majeshi awauliza ninyi, enyi makuhani, mnaolidharau jina langu. Nanyi mwasema, Tumelidharau jina lako kwa jinsi gani?


Wala msiitwe viongozi; maana Kiongozi wenu ni mmoja, naye ndiye Kristo.


Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote.


Basi ikiwa ninyi, mlio waovu, mnajua kuwapa watoto wenu zawadi njema, je! Si Baba yenu aliye mbinguni atawapa mema zaidi wao wamwombao?


Akasema, Enyi wanaume, ndugu zangu na baba zangu, nisikilizeni, nikijitetea mbele yenu sasa.


Kwa kuwa ijapokuwa mna waalimu elfu kumi katika Kristo, lakini hamna baba wengi. Maana mimi ndimi niliyewazaa katika Kristo Yesu kwa njia ya Injili.


Nitakuwa Baba kwenu, Nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike, asema Bwana Mwenyezi.


Na pamoja na hayo tulikuwa na baba zetu wa mwili walioturudi, nasi tukawaheshimu; basi si ni afadhali zaidi kujitia chini ya Baba wa roho zetu na kuishi?


Tazameni, ni pendo la namna gani alilotupa Baba, kwamba tuitwe wana wa Mungu; na ndivyo tulivyo. Kwa sababu hii ulimwengu haututambui, kwa kuwa haukumtambua yeye.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo