Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Isaya 44:5 - Swahili Revised Union Version

5 Mmoja atasema, Mimi ni wa BWANA; na mwingine atajiita kwa jina la Yakobo; na mwingine ataandika juu ya mkono wake, Kwa BWANA, na kujiita kwa jina la Israeli.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 “Mmoja atasema: ‘Mimi ni wa Mwenyezi-Mungu’, mwingine atajiita kwa jina la Yakobo, mwingine ataandika mkononi mwake, ‘Wa Mwenyezi-Mungu’, na kujitambulisha kwa jina la Israeli.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

5 “Mmoja atasema: ‘Mimi ni wa Mwenyezi-Mungu’, mwingine atajiita kwa jina la Yakobo, mwingine ataandika mkononi mwake, ‘Wa Mwenyezi-Mungu’, na kujitambulisha kwa jina la Israeli.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 “Mmoja atasema: ‘Mimi ni wa Mwenyezi-Mungu’, mwingine atajiita kwa jina la Yakobo, mwingine ataandika mkononi mwake, ‘Wa Mwenyezi-Mungu’, na kujitambulisha kwa jina la Israeli.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 Mmoja atasema, ‘Mimi ni wa Mwenyezi Mungu’; mwingine atajiita kwa jina la Yakobo; vilevile mwingine ataandika juu ya mkono wake, ‘Wa Mwenyezi Mungu,’ na kujiita kwa jina la Israeli.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 Mmoja atasema, ‘Mimi ni wa bwana’; mwingine atajiita kwa jina la Yakobo; vilevile mwingine ataandika juu ya mkono wake, ‘Wa bwana,’ na kujiita kwa jina la Israeli.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

5 Mmoja atasema, Mimi ni wa BWANA; na mwingine atajiita kwa jina la Yakobo; na mwingine ataandika juu ya mkono wake, Kwa BWANA, na kujiita kwa jina la Israeli.

Tazama sura Nakili




Isaya 44:5
16 Marejeleo ya Msalaba  

Koreshi, mfalme wa Uajemi asema hivi; BWANA, Mungu wa mbinguni, amenipa falme zote za dunia; naye ameniagiza nimjengee nyumba katika Yerusalemu, ulioko Yuda. Basi kila mtu katika ninyi nyote mlio watu wake, BWANA, Mungu wake, na awe pamoja naye, na akwee.


Na kwa sababu ya hayo yote sisi tunafanya agano la hakika, na kuliandika; na wakuu wetu, na Walawi wetu, na makuhani wetu, wanalitilia mhuri.


Ee BWANA, hakika mimi ni mtumishi wako, Mtumishi wako, mwana wa mjakazi wako, Umevifungua vifungo vyangu.


Nayo itakuwa ishara kwako katika mkono wako, na kwa ukumbusho kati ya macho yako, ili kwamba sheria ya BWANA ipate kuwa kinywani mwako; kwani BWANA alikuondoa utoke Misri kwa mkono wenye uwezo.


Na mataifa mengi watakwenda na kusema, Njoni, twende juu mlimani kwa BWANA, nyumbani kwa Mungu wa Yakobo, naye atatufundisha njia zake, nasi tutakwenda katika mapito yake maana katika Sayuni itatoka sheria, na neno la BWANA katika Yerusalemu.


Nami nikaitia sahihi ile hati, na kuipiga mhuri, nikawaita mashahidi, nikampimia ile fedha katika mizani.


Watauliza njia ya kwenda Sayuni, na nyuso zao zitaelekea huko, wakisema, Njooni ninyi, mjiunge na BWANA, kwa agano la milele ambalo halitasahauliwa.


Na mataifa mengi watakwenda na kusema, Njooni, twende juu mlimani kwa BWANA, na nyumbani kwa Mungu wa Yakobo; naye atatufundisha njia zake, nasi tutakwenda katika mapito yake; kwa maana katika Sayuni itatoka sheria, na neno la BWANA litatoka Yerusalemu.


Nami nitalileta fungu lile la tatu na kulipitisha kati ya moto, nami nitawasafisha kama fedha isafishwavyo, nami nitawajaribu kama dhahabu ijaribiwavyo; wataliitia jina langu, nami nitawasikia; mimi nitasema, Watu hawa ndio wangu; nao watasema, BWANA ndiye Mungu wangu.


Tena walitenda hivi si kama tulivyotumaini tu, bali kwanza walijitoa nafsi zao kwa Bwana; na kwetu pia, kwa mapenzi ya Mungu.


Na wote watakaoenenda kwa kanuni hiyo, amani na iwe kwao na rehema, naam, kwa Israeli wa Mungu.


Tangu sasa mtu asinitaabishe; kwa maana ninachukua mwilini mwangu chapa zake Yesu.


Bali ninyi ni uzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo