Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Isaya 17:3 - Swahili Revised Union Version

3 Na ngome ya Efraimu itakomeshwa, na ufalme wa Dameski, na mabaki ya Shamu; watakuwa kama utukufu wa wana wa Israeli, asema BWANA wa majeshi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 Ngome za kujihami za Efraimu zitatoweka, na utawala wa Damasko utakwisha. Waashuru ambao watabaki hai, watakuwa na fedheha kama wazawa wa Israeli. Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nimenena.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

3 Ngome za kujihami za Efraimu zitatoweka, na utawala wa Damasko utakwisha. Waashuru ambao watabaki hai, watakuwa na fedheha kama wazawa wa Israeli. Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nimenena.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 Ngome za kujihami za Efraimu zitatoweka, na utawala wa Damasko utakwisha. Waashuru ambao watabaki hai, watakuwa na fedheha kama wazawa wa Israeli. Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nimenena.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 Mji wenye ngome utatoweka kutoka Efraimu, nao uweza wa ufalme kutoka Dameski; mabaki ya Aramu yatakuwa kama utukufu wa Waisraeli,” asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

3 Mji wenye ngome utatoweka kutoka Efraimu, nao uweza wa ufalme kutoka Dameski; mabaki ya Aramu yatakuwa kama utukufu wa Waisraeli,” asema bwana Mwenye Nguvu Zote.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

3 Na ngome ya Efraimu itakomeshwa, na ufalme wa Dameski, na mabaki ya Shamu; watakuwa kama utukufu wa wana wa Israeli, asema BWANA wa majeshi.

Tazama sura Nakili




Isaya 17:3
27 Marejeleo ya Msalaba  

Na huyo mfalme wa Ashuru akamsikia; mfalme wa Ashuru akapanda juu ya Dameski, akautwaa, akawahamisha watu wake mateka mpaka Kiri, akamwua Resini.


Katika mwaka wa tisa wa Hoshea, huyo mfalme wa Ashuru akautwaa Samaria, akawahamisha Israeli mpaka Ashuru, akawaweka katika Hala na Habori, karibu na mto wa Gozani, na katika miji ya Wamedi.


Je! Kalno si kama Karkemishi? Hamathi si kama Arpadi? Samaria si kama Dameski?


Lakini sasa BWANA asema hivi, Katika muda wa miaka mitatu, kama miaka ya mtu wa mshahara, utukufu wa Moabu utadharauliwa, licha ya wingi wa watu wake; na watakaobaki watakuwa wachache sana na dhaifu.


Tena itakuwa katika siku hiyo, utukufu wa Yakobo utapungua na kunona kwa mwili wake kutakwisha.


Kwa sababu umefanya mji kuwa ni rundo; Mji wenye boma kuwa ni magofu; Jumba la wageni kuwa si mji; Hautajengwa tena milele.


Kwa maana kabla mtoto huyo hajajua kuyakataa mabaya na kuyachagua mema, nchi ile, ambayo wewe unawachukia wafalme wake wawili, itaachwa ukiwa.


Kwa maana kichwa cha Shamu ni Dameski, na kichwa cha Dameski ni Resini; na katika muda wa miaka sitini na mitano Efraimu atavunjika vipande vipande, asiwe kabila la watu tena;


Kwa maana kabla mtoto huyo hajaweza kujua kusema, Baba yangu, na Mama yangu, hazina za Dameski na mateka ya Samaria yatachukuliwa mbele ya mfalme wa Ashuru.


BWANA akamwambia, Mwite jina lake Yezreeli; kwa maana bado kitambo kidogo, nitaipatiliza nyumba ya Yehu damu ya Yezreeli, na kuukomesha ufalme wa nyumba ya Israeli.


Akachukua mimba tena, akazaa mtoto wa kike, BWANA akamwambia, Mwite jina lake Lo-ruhama; kwa maana sitairehemu nyumba ya Israeli tena, nisije nikawasamehe kwa njia yoyote.


Kwa sababu hiyo fitina itatokea kati ya watu wako, na ngome zako zote zitaharibiwa, kama vile Shalmani alivyoharibu Betharbeli, katika siku ya vita; mama akavunjikavunjika pamoja na watoto wake.


Kwa maana wana wa Israeli watakaa siku nyingi bila mfalme, wala mtu mkuu, wala sadaka, wala nguzo, wala naivera, wala kinyago;


Israeli amemezwa; sasa wamo miongoni mwa mataifa kama chombo kisichopendeza.


Naye Efraimu, utukufu wake utarukia mbali kama ndege, uzazi hautakuwako, wala aliye na mimba, wala achukuaye mimba.


Na hao waapao kwa dhambi ya Samaria, na kusema, Kama aishivyo Mungu wako, Ee Dani, na, Kama iishivyo njia ya Beer-sheba, hao nao wataanguka, wasiinuke tena.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo