Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Isaya 1:11 - Swahili Revised Union Version

11 Huu wingi wa sadaka zenu mnazonitolea una faida gani? Asema BWANA. Nimejaa mafuta ya kafara za kondoo dume, na mafuta ya wanyama walionona; nami siifurahii damu ya ng'ombe wala ya wana-kondoo wala ya mbuzi dume.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 Mwenyezi-Mungu asema hivi; “Wingi wa tambiko zenu ni kitu gani kwangu? Nimezichoka sadaka zenu za kondoo wa kuteketezwa na mafuta ya wanyama wenu wanono. Sipendezwi na damu ya fahali, wala ya wanakondoo, wala ya beberu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 Mwenyezi-Mungu asema hivi; “Wingi wa tambiko zenu ni kitu gani kwangu? Nimezichoka sadaka zenu za kondoo wa kuteketezwa na mafuta ya wanyama wenu wanono. Sipendezwi na damu ya fahali, wala ya wanakondoo, wala ya beberu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 Mwenyezi-Mungu asema hivi; “Wingi wa tambiko zenu ni kitu gani kwangu? Nimezichoka sadaka zenu za kondoo wa kuteketezwa na mafuta ya wanyama wenu wanono. Sipendezwi na damu ya fahali, wala ya wanakondoo, wala ya beberu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 Mwenyezi Mungu anasema, “Wingi wa sadaka zenu, ni kitu gani kwangu? Nina sadaka za kuteketezwa nyingi kupita kiasi, za kondoo dume na mafuta ya wanyama walionona. Sipendezwi na damu za mafahali wala za wana-kondoo na mbuzi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 bwana anasema, “Wingi wa sadaka zenu, ni kitu gani kwangu? Ninazo sadaka za kuteketezwa nyingi kupita kiasi, za kondoo dume na mafuta ya wanyama walionona. Sipendezwi na damu za mafahali wala za wana-kondoo na mbuzi.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

11 Huu wingi wa sadaka zenu mnazonitolea una faida gani? Asema BWANA. Nimejaa mafuta ya kafara za kondoo dume, na mafuta ya wanyama walionona; nami siifurahii damu ya ng'ombe wala ya wana-kondoo wala ya mbuzi dume.

Tazama sura Nakili




Isaya 1:11
23 Marejeleo ya Msalaba  

Dhabihu na matoleo hukupendezwa nazo, Umetuzidishia ila masikio, Kafara na sadaka za dhambi hukuzitaka.


Sitakukemea kwa ajili ya dhabihu zako, Na kafara zako ziko mbele zangu daima.


Maana hupendezwi na dhabihu, na kama ningeitoa, Wewe huridhii sadaka ya kuteketezwa.


Sadaka ya mtu mbaya ni chukizo kwa BWANA; Bali maombi ya mtu mnyofu ni furaha yake.


Sadaka ya wasio haki ni chukizo; Si zaidi sana ailetapo mwenye nia mbaya!


Kutenda haki na hukumu Humpendeza BWANA kuliko kutoa sadaka.


Walakini wanitafuta kila siku; hupenda kujua njia zangu; kama vile taifa waliotenda haki, wasioacha sheria ya Mungu wao, hutaka kwangu amri za haki; hufurahi kumkaribia Mungu.


Yeye achinjaye ng'ombe ni kama yeye amwuaye mtu; na yeye atoaye dhabihu ya mwana-kondoo ni kama yeye avunjaye shingo ya mbwa; na yeye atoaye matoleo ni kama yeye atoaye damu ya nguruwe; na yeye afukizaye uvumba ni kama yeye abarikiye sanamu; naam, wamezichagua njia zao wenyewe, na nafsi zao zafurahia machukizo yao.


Yafaa nini niletewe ubani kutoka Sheba, na udi kutoka nchi iliyo mbali? Sadaka zenu za kuteketezwa hazikubaliwi, wala dhabihu zenu haziniridhii.


BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Tieni sadaka zenu za kuteketezwa pamoja na dhabihu zenu, mkale nyama.


Maana nataka fadhili wala si sadaka; na kumjua Mungu kuliko sadaka za kuteketezwa.


Kwa habari za dhabihu za matoleo yangu, hutoa dhabihu ya nyama na kuila; lakini BWANA hawakubali; sasa ataukumbuka uovu wao, na kuwapatiliza dhambi zao; watarudi kwenda Misri.


mkachome sadaka ya shukrani, ya kitu kilichotiwa chachu; mkatangaze sadaka mtoazo kwa hiari na kuzihubiri habari zake; kwa maana ndivyo viwapendezavyo ninyi, enyi wana wa Israeli, asema Bwana MUNGU.


Mimi nazichukia sikukuu zenu, nazidharau, nami sitapendezwa na makutano yenu ya dini.


Naam, ijapokuwa mnanitolea sadaka zenu za kuteketezwa na sadaka zenu za unga, sitazikubali; wala sitaziangalia sadaka zenu za amani, na za wanyama walionona.


Je! BWANA atapendezwa na maelfu ya kondoo dume, au na makumi elfu ya mito ya mafuta? Je! Nimtoe mzaliwa wangu wa kwanza kwa kosa langu, mzawa wa mwili wangu kwa dhambi ya roho yangu?


Ndipo Hagai akajibu, akasema, Hivyo ndivyo walivyo watu hawa, na hivyo ndivyo lilivyo taifa hili mbele zangu, asema BWANA; na hivyo ndivyo ilivyo kila kazi ya mikono yao; na kitu hicho wakitoacho sadaka huko ni najisi.


Waambie watu wote wa nchi, na hao makuhani, ukisema, Hapo mlipofunga na kuomboleza katika mwezi wa tano na mwezi wa saba, katika miaka hiyo sabini, je, Mlifunga kwa ajili yangu?


Laiti angekuwapo kwenu mtu mmoja wa kuifunga milango; msije mkawasha moto bure madhabahuni pangu! Sina furaha kwenu, asema BWANA wa majeshi, wala sitakubali dhabihu yoyote mikononi mwenu.


na ng'ombe dume mchanga mmoja, na kondoo dume mmoja, na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kuwa sadaka ya kuteketezwa;


Akatuma tena watu kwa wengine, akisema, Waambieni wale walioalikwa, Tazameni, nimeandaa karamu yangu; ng'ombe zangu na vinono vimekwisha kuchinjwa, na vyote vimekuwa tayari, njoni arusini.


Lakini nendeni, mkajifunze maana yake maneno haya, Nataka rehema, wala si sadaka; kwa maana sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi.


Naye Samweli akasema, Je! BWANA huzipenda sadaka za kuteketezwa na dhabihu Sawasawa na kuitii sauti ya BWANA? Angalia, kutii ni bora kuliko dhabihu, Na kusikiza ushauri kuliko mafuta ya beberu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo