Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Hosea 7:12 - Swahili Revised Union Version

12 Watakapokwenda nitatandika wavu wangu juu yao; nitawashusha kama ndege wa angani; nitawarudi, kama vile mkutano wao ulivyosikia.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

12 Watakapokwenda nitatandaza wavu wangu niwanase, nitawaangusha chini kama ndege wa angani; nitamwaadhibu kadiri ya ripoti ya maovu yao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

12 Watakapokwenda nitatandaza wavu wangu niwanase, nitawaangusha chini kama ndege wa angani; nitamwaadhibu kadiri ya ripoti ya maovu yao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

12 Watakapokwenda nitatandaza wavu wangu niwanase, nitawaangusha chini kama ndege wa angani; nitamwaadhibu kadiri ya ripoti ya maovu yao.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

12 Watakapoenda, nitatupa wavu wangu juu yao; nitawavuta chini waanguke kama ndege wa angani. Nitakaposikia wakikusanyika pamoja, nitawanasa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

12 Wakati watakapokwenda, nitatupa wavu wangu juu yao; nitawavuta chini waanguke kama ndege wa angani. Nitakaposikia wakikusanyika pamoja, nitawanasa.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

12 Watakapokwenda nitatandika wavu wangu juu yao; nitawashusha kama ndege wa angani; nitawarudi, kama vile mkutano wao ulivyosikia.

Tazama sura Nakili




Hosea 7:12
15 Marejeleo ya Msalaba  

Jueni basi kuwa Mungu amenipotosha, Na kunizingira kwa wavu wake.


Maana mwanadamu naye hajui wakati wake; kama samaki wanaokamatwa katika nyavu mbaya, na mfano wa ndege wanaonaswa mtegoni, kadhalika wanadamu hunaswa katika wakati mbaya, unapowaangukia kwa ghafla.


Tazama, asema BWANA, Nitatuma watu kuwaita wavuvi wengi, nao watawavua; na baada ya hayo nitatuma watu kuwaita wawindaji wengi, nao watawawinda, watoke katika kila mlima, na kila kilima, na pango za majabali.


Tena nilituma kwenu watumishi wangu wote, manabii, nikiamka mapema na kuwatuma, nikisema, Basi ninyi; msilifanye chukizo hili linalochukiza.


Tena wavu wangu nitautandika juu yake, naye atanaswa kwa mtego wangu; nami nitampeleka Babeli, mpaka nchi ya Wakaldayo; lakini hataiona, ingawa atakufa huko.


Nami nitatandika wavu wangu juu yake, naye atanaswa katika mtego wangu, nami nitamleta hadi Babeli; nami nitateta naye huko kwa sababu ya kosa lake alilonikosa.


Bwana MUNGU asema hivi; Nitautanda wavu wangu juu yako, kwa kusanyiko la watu wa kabila nyingi; nao watakuvua katika jarife langu.


Efraimu atakuwa ukiwa siku ya adhabu; katika makabila ya Israeli nimetangaza jambo litakalotukia kweli.


Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo