Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Hesabu 9:6 - Swahili Revised Union Version

6 Basi walikuwako wanaume kadhaa waliokuwa na unajisi kwa ajili ya maiti wa mtu, hata wasiweze kuishika Pasaka siku hiyo; nao wakaenda mbele ya Musa na Haruni, siku hiyo hao watu wakamwambia,

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

6 Lakini, baadhi ya watu waliokuwapo walikuwa hawawezi kuiadhimisha sikukuu hiyo ya Pasaka kwa sababu walikuwa wamegusa maiti, wakawa najisi. Hao waliwaendea Mose na Aroni,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

6 Lakini, baadhi ya watu waliokuwapo walikuwa hawawezi kuiadhimisha sikukuu hiyo ya Pasaka kwa sababu walikuwa wamegusa maiti, wakawa najisi. Hao waliwaendea Mose na Aroni,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

6 Lakini, baadhi ya watu waliokuwapo walikuwa hawawezi kuiadhimisha sikukuu hiyo ya Pasaka kwa sababu walikuwa wamegusa maiti, wakawa najisi. Hao waliwaendea Mose na Aroni,

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

6 Lakini baadhi yao hawakuweza kuadhimisha Pasaka siku ile kwa sababu walikuwa najisi kwa ajili ya kugusa maiti. Kwa hiyo wakamwendea Musa na Haruni siku ile ile,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

6 Lakini baadhi yao hawakuweza kuadhimisha Pasaka siku ile kwa sababu walikuwa najisi kwa taratibu za kiibada kwa ajili ya kugusa maiti. Kwa hiyo wakamwendea Musa na Haruni siku ile ile,

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

6 Basi walikuwako wanaume kadhaa waliokuwa na unajisi kwa ajili ya maiti wa mtu, hata wasiweze kuishika Pasaka siku hiyo; nao wakaenda mbele ya Musa na Haruni, siku hiyo hao watu wakamwambia,

Tazama sura Nakili




Hesabu 9:6
16 Marejeleo ya Msalaba  

Musa akamwambia mkwewe, Ni kwa sababu watu hunijilia mimi wapate kumwuliza Mungu;


Sikiza sasa neno langu, nitakupa shauri, na Mungu na awe pamoja nawe; uwe wewe kwa ajili ya watu mbele ya Mungu, nawe umletee Mungu maneno yao;


Nao wakawaamua watu sikuzote; mashauri magumu wakamletea Musa, lakini kila neno dogo wakaliamua wenyewe.


wala hataingia penye maiti, wala asijitie unajisi kwa ajili ya baba yake wala mama yake;


kisha huyo mwanamume ambaye mama ni Mwisraeli akakufuru jina la Bwana na kulaani nao watu wakampeleka kwa Musa. Mama yake mtu huyo alikuwa akiitwa Shelomithi, binti ya Dibri, wa kabila la Dani.


Hao waliomwona akikusanya kuni wakamleta kwa Musa na Haruni, na kwa mkutano wote.


Mtu agusaye maiti yeyote atakuwa najisi muda wa siku saba;


Hii ndiyo amri, mtu afapo ndani ya hema; kila mtu aingiaye ndani ya hema hiyo, na kila mtu aliye humo hemani, atakuwa najisi muda wa siku saba.


Kisha mtu yeyote huko nje shambani atakayemgusa mtu aliyeuawa kwa upanga, au mzoga, au mfupa wa mtu, au kaburi, atakuwa najisi muda wa siku saba.


kisha mtu mmoja aliye safi atatwaa hisopo, na kuitia katika hayo maji naye atayanyunyiza juu ya hema, na juu ya vyombo vyote, na juu ya watu waliokuwapo, na juu yake yeye aliyeugusa mfupa, au mtu aliyeuawa, au mzoga, au kaburi;


Nao wakasimama mbele ya Musa, na mbele ya Eleazari kuhani, na mbele ya wakuu, na mkutano wote, mlangoni pa hema ya kukutania, wakasema,


Basi Musa akaleta neno lao mbele ya BWANA


Waamrishe wana wa Israeli kwamba wamtoe kila mwenye ukoma kambini, na kila mtu aliye na kisonono, na kila aliye najisi kwa ajili ya maiti;


Sisi tuko katika hali ya unajisi kwa ajili ya maiti wa mtu; nasi tumezuiwa kwa nini hata tusipate kumtolea BWANA matoleo kwa wakati wake ulioagizwa, kati ya wana wa Israeli?


Kisha wakamchukua Yesu kutoka kwa Kayafa mpaka Praitorio, nayo ikawa alfajiri; lakini wao wenyewe hawakuingia ndani ya ile Praitorio, wasije wakanajisika, bali wapate kuila Pasaka.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo