Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Hesabu 9:5 - Swahili Revised Union Version

5 Nao wakaiadhmisha Pasaka katika mwezi wa kwanza, siku ya kumi na nne ya mwezi, wakati wa jioni, katika bara ya Sinai vile vile kama hayo yote BWANA aliyomwagiza Musa, ndivyo walivyofanya wana wa Israeli.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 Basi, wakaiadhimisha Pasaka jioni, siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza, katika jangwa la Sinai. Waisraeli walifanya yote kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Mose.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

5 Basi, wakaiadhimisha Pasaka jioni, siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza, katika jangwa la Sinai. Waisraeli walifanya yote kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Mose.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 Basi, wakaiadhimisha Pasaka jioni, siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza, katika jangwa la Sinai. Waisraeli walifanya yote kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Mose.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 nao wakafanya hivyo kwenye Jangwa la Sinai wakati wa kuzama jua siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza. Waisraeli wakafanya kila kitu kama vile Mwenyezi Mungu alivyomwamuru Musa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 nao wakafanya hivyo kwenye Jangwa la Sinai wakati wa kuzama jua siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza. Waisraeli wakafanya kila kitu kama vile bwana alivyomwamuru Musa.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

5 Nao wakaiadhimisha Pasaka katika mwezi wa kwanza, siku ya kumi na nne ya mwezi, wakati wa jioni, katika bara ya Sinai vile vile kama hayo yote BWANA aliyomwagiza Musa, ndivyo walivyofanya wana wa Israeli.

Tazama sura Nakili




Hesabu 9:5
18 Marejeleo ya Msalaba  

Ndivyo alivyofanya Nuhu, sawasawa na vyote alivyomwamuru Mungu, hivyo ndivyo alivyofanya.


Nuhu akafanya kama vile BWANA alivyomwamuru.


Ndivyo walivyofanya wana wa Israeli wote; kama BWANA alivyowaagiza Musa na Haruni, ndivyo walivyofanya.


Basi ndivyo ilivyomalizwa kazi yote ya maskani ya hema ya kukutania; na wana wa Israeli walifanya kama yote BWANA aliyomwagiza Musa, ndivyo walivyofanya.


Sawasawa na yote BWANA aliyomwagiza Musa, ndivyo walivyoifanya hiyo kazi yote wana wa Israeli.


Ndivyo walivyofanya wana wa Israeli; kama yote BWANA aliyomwagiza Musa, ndivyo walivyofanya.


Naye Musa akawaambia wana wa Israeli vile vile kama hayo yote BWANA alivyomwagiza Musa.


Basi Musa na Haruni, na mkutano wote wa wana wa Israeli, wakawafanyia Walawi mambo hayo; kama hayo yote BWANA aliyomwagiza Musa kwa habari za hao Walawi, ndivyo wana wa Israeli walivyowafanyia.


Kisha Musa akawaambia wana wa Israeli kwamba waadhimishe sikukuu hiyo ya Pasaka;


na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.


Ninyi mmekuwa rafiki zangu, mkitenda niwaamuruyo.


Kwa hiyo, Ee Mfalme Agripa, sikuyaasi yale maono ya mbinguni,


Ikawa mwaka wa arubaini, mwezi wa kumi na moja, siku ya kwanza ya mwezi, Musa akawaambia wana wa Israeli kama yote aliyopewa na BWANA ya kuwaamuru;


Angalieni nimewafundisha amri na hukumu, vile vile kama BWANA, Mungu wangu, alivyoniamuru, ili mzitende katika nchi mwingiayo ili kuimiliki.


Kwa imani Abrahamu alipoitwa aliitika, atoke aende mahali pale atakapopapata kuwa urithi; akatoka asijue aendako.


Na Musa kweli alikuwa mwaminifu katika nyumba yote ya Mungu kama mtumishi, awe ushuhuda wa mambo yatakayonenwa baadaye;


Basi wana wa Israeli wakapanga hema zao huko Gilgali; nao wakala sikukuu ya Pasaka siku ya kumi na nne ya mwezi, jioni, katika nchi tambarare za Yeriko.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo