Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Hesabu 6:5 - Swahili Revised Union Version

5 Siku zote za nadhiri yake ya kujitenga, wembe usimguse kichwani mwake; hata hizo siku zitakapotimia, ambazo alijiweka wakfu kwa BWANA, atakuwa mtakatifu, ataziacha nywele za kichwani mwake zikue ziwe ndefu.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 “Siku zote za nadhiri yake ya kujitenga, hatanyoa nywele zake; mpaka muda wa nadhiri yake ya kujiweka wakfu kwa Mwenyezi-Mungu utakapomalizika, atakuwa mtakatifu, ataziacha nywele zake ziwe ndefu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

5 “Siku zote za nadhiri yake ya kujitenga, hatanyoa nywele zake; mpaka muda wa nadhiri yake ya kujiweka wakfu kwa Mwenyezi-Mungu utakapomalizika, atakuwa mtakatifu, ataziacha nywele zake ziwe ndefu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 “Siku zote za nadhiri yake ya kujitenga, hatanyoa nywele zake; mpaka muda wa nadhiri yake ya kujiweka wakfu kwa Mwenyezi-Mungu utakapomalizika, atakuwa mtakatifu, ataziacha nywele zake ziwe ndefu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 “ ‘Kwa muda wote wa nadhiri yake ya kujitenga kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, wembe hautapita kichwani mwake. Ni lazima awe mtakatifu hadi kipindi cha kujitenga kwake kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kiishe; ni lazima aache nywele za kichwa chake zirefuke.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 “ ‘Kwa muda wote wa nadhiri yake ya kujitenga kwa ajili ya bwana, wembe hautapita kichwani mwake. Ni lazima awe mtakatifu mpaka kipindi cha kujitenga kwake kwa ajili ya bwana kiishe; ni lazima aache nywele za kichwa chake zirefuke.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

5 Siku zote za nadhiri yake ya kujitenga, wembe usimguse kichwani mwake; hata hizo siku zitakapotimia, ambazo alijiweka wakfu kwa BWANA, atakuwa mtakatifu, ataziacha nywele za kichwani mwake zikue ziwe ndefu.

Tazama sura Nakili

Hesabu 6:5
9 Marejeleo ya Msalaba  

Hawatanyoa vichwa vyao, wala hawataacha nywele zao kuwa ndefu sana; watazipunguza nywele za vichwa vyao tu.

Siku zote za kujitenga kwake asile kitu chochote kilichoandaliwa kwa mzabibu, tangu kokwa hata maganda.

Baada ya hayo Paulo akazidi kukaa huko siku nyingi, kisha akaagana na ndugu akaabiri kwenda Shamu; na Priskila na Akila wakaenda pamoja naye, alipokwisha kunyoa kichwa chake huko Kenkrea; maana alikuwa ana nadhiri.

kwani tazama, utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto mwanamume; na wembe usipite juu ya kichwa chake; maana mtoto huyo atakuwa mnadhiri wa Mungu tangu tumboni; naye ataanza kuwaokoa Israeli na mikono ya Wafilisti.

Ndipo alipomwambia yote yaliyokuwa moyoni mwake, akamwambia, Wembe haukupita juu ya kichwa changu kamwe; maana mimi nimekuwa Mnadhiri wa Mungu, tangu tumboni mwa mama yangu; nikinyolewa, ndipo nguvu zangu zitanitoka, nami nitakuwa dhaifu, nitakuwa kama wanadamu wenzangu.

Naye akamlaza usingizi magotini pake. Kisha akamwita mtu akavinyoa vile vishungi saba vya nywele za kichwa chake; akaanza kumsumbua, nguvu zake zikamtoka.

Akaweka nadhiri, akasema, Ee BWANA wa majeshi, ikiwa wewe utayaangalia mateso la mjakazi wako, na kunikumbuka, wala usinisahau mimi mjakazi wako, na kunipa mimi mjakazi wako mtoto wa kiume, ndipo mimi nitakapompa BWANA huyo mtoto siku zote za maisha yake, wala wembe hautamfikia kichwani kamwe.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo