Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Hesabu 5:9 - Swahili Revised Union Version

9 Tena kila sadaka ya kuinuliwa, ya vitu vitakatifu vya wana wa Israeli, watakavyovileta kwa kuhani, vitakuwa ni vyake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 Michango yote na matoleo yote ambayo Waisraeli wataweka wakfu kwa Mungu na kumletea kuhani itakuwa yake huyo kuhani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

9 Michango yote na matoleo yote ambayo Waisraeli wataweka wakfu kwa Mungu na kumletea kuhani itakuwa yake huyo kuhani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 Michango yote na matoleo yote ambayo Waisraeli wataweka wakfu kwa Mungu na kumletea kuhani itakuwa yake huyo kuhani.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 Matoleo yote matakatifu ya Waisraeli wanayoleta kwa kuhani yatakuwa yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

9 Matoleo yote matakatifu ya Waisraeli wanayoleta kwa kuhani yatakuwa yake.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

9 Tena kila sadaka ya kuinuliwa, ya vitu vitakatifu vya wana wa Israeli, watakavyovileta kwa kuhani, vitakuwa ni vyake.

Tazama sura Nakili




Hesabu 5:9
19 Marejeleo ya Msalaba  

navyo vitakuwa vya Haruni na wanawe posho ya lazima sikuzote itokayo kwa hao wana wa Israeli; kwa kuwa ni sadaka ya kuinuliwa; nayo itakuwa ni sadaka ya kuinuliwa itokayo kwa hao wana wa Israeli katika dhabihu zao za sadaka za amani, ni sadaka yao ya kuinuliwa kwa ajili ya BWANA.


nanyi mtaila katika mahali patakatifu, kwa sababu ni haki yako, na haki ya wanao, katika hizo kafara zisongezwazo kwa BWANA kwa moto; kwani niliagizwa hivyo.


Na kidari cha kutikiswa, na mguu wa kuinuliwa, mtavila katika mahali palipo safi; wewe, na wanao, na binti zako pamoja nawe; kwa maana vimetolewa kuwa ni haki yako, na haki ya wanao, katika zile kafara za sadaka za amani za wana wa Israeli.


Mguu wa kuinuliwa, na kidari cha kutikiswa, Watavileta pamoja na dhabihu zisongezwazo kwa njia ya moto, za hayo mafuta ili kuvitikisa viwe sadaka ya kutikiswa mbele za BWANA; kisha vitakuwa ni vyako wewe, na vya wanao pamoja nawe, ni haki yenu milele, kama BWANA alivyoagiza.


Huyo kuhani atakayeisongeza kwa ajili ya dhambi ndiye atakayeila; italiwa katika mahali patakatifu, katika ua wa hema ya kukutania.


Mguu wa nyuma wa upande wa kulia mtampa kuhani kuwa sadaka ya kuinuliwa kutoka kwa hizo sadaka zenu za amani.


Kwa maana, hicho kidari cha kutikiswa, na huo mguu wa kuinuliwa, nimevitwaa kwa wana wa Israeli, katika dhabihu zao za sadaka za amani, nami nimempa Haruni kuhani na wanawe, kuwa haki yao ya milele kutoka kwa wana wa Israeli.


Sadaka zote za kuinuliwa za vitu vitakatifu, wana wa Israeli wavisongezavyo kwa BWANA, nimekupa wewe na wanao na binti zako pamoja nawe, ni haki yenu ya milele; ni agano la chumvi la milele mbele za BWANA kwa ajili yako, na kizazi chako pamoja nawe.


Basi Musa akampa Eleazari kuhani hiyo sehemu, iliyokuwa sadaka ya kuinuliwa kwa BWANA, kama BWANA alivyomwagiza Musa.


Lakini ikiwa mtu huyo hana jamaa ya karibu ambaye inampasa kurudishiwa kwa ajili ya hiyo hatia, kile kitakachorudishwa kwa BWANA kwa hiyo hatia kitakuwa cha kuhani, pamoja na kondoo dume wa upatanisho, ambaye kwa huyo utafanywa upatanisho kwa ajili yake.


Ila vitu vyako vitakatifu ulivyo navyo, na nadhiri zako, uvitwae uende mahali atakapochagua BWANA;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo