Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Hesabu 22:18 - Swahili Revised Union Version

18 Balaamu akajibu akawaambia watumishi wa Balaki, Hata kama Balaki angenipa nyumba yake imejaa fedha na dhahabu, siwezi kukiuka neno la BWANA, Mungu wangu, kulipunguza au kuliongeza.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

18 Lakini Balaamu akawajibu watumishi wa Balaki, “Hata kama Balaki atanipa nyumba yake imejaa fedha na dhahabu, mimi sitaweza kuvunja amri ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu, kuhusu jambo lolote, dogo au kubwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

18 Lakini Balaamu akawajibu watumishi wa Balaki, “Hata kama Balaki atanipa nyumba yake imejaa fedha na dhahabu, mimi sitaweza kuvunja amri ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu, kuhusu jambo lolote, dogo au kubwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

18 Lakini Balaamu akawajibu watumishi wa Balaki, “Hata kama Balaki atanipa nyumba yake imejaa fedha na dhahabu, mimi sitaweza kuvunja amri ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu, kuhusu jambo lolote, dogo au kubwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

18 Lakini Balaamu akawajibu, “Hata kama Balaki angenipa jumba lake la kifalme likiwa limejazwa fedha na dhahabu, singeweza kufanya kitu chochote kikubwa au kidogo ili kutenda kitu nje ya agizo la Mwenyezi Mungu, Mungu wangu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

18 Lakini Balaamu akawajibu, “Hata kama Balaki angenipa jumba lake la kifalme likiwa limejazwa fedha na dhahabu, singeweza kufanya kitu chochote kikubwa au kidogo ili kutenda kitu nje ya agizo la bwana Mwenyezi Mungu wangu.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

18 Balaamu akajibu akawaambia watumishi wa Balaki, Hata kama Balaki angenipa nyumba yake imejaa fedha na dhahabu, siwezi kukiuka neno la BWANA, Mungu wangu, kulipunguza au kuliongeza.

Tazama sura Nakili

Hesabu 22:18
14 Marejeleo ya Msalaba  

Mtu wa Mungu akamwambia mfalme, Ujaponipa nusu ya nyumba yako, sitaingia pamoja nawe, wala sitakula chakula, wala sitakunywa maji mahali hapa;

Mikaya akasema, Kama BWANA aishivyo, neno lile BWANA aniambialo, ndilo nitakalolinena.

Mikaya akasema, Kama aishivyo BWANA, neno lile atakalolinena Mungu wangu, ndilo nitakalolinena.

Au pamoja na wakuu wenye dhahabu, Waliozijaza nyumba zao fedha;

Ndipo Danieli akajibu, akasema mbele ya mfalme; Zawadi zako baki nazo wewe mwenyewe; na thawabu zako mpe mtu mwingine; lakini nitamsomea mfalme maandiko haya, na kumjulisha tafsiri yake.

Basi sasa nawasihi, kaeni hapa tena usiku huu, nipate kujua BWANA atakaloniambia zaidi.

Balaamu akamwambia Balaki, Tazama, nimekujia. Je! Mimi sasa nina uwezo wowote kusema neno lolote? Neno lile Mungu atakalolitia kinywani mwangu, ndilo nitakalolisema.

Akawaambia, Kaeni hapa usiku huu, nami nitawaletea jawabu kama BWANA atakavyoniambia; wakuu wa Moabu wakakaa na Balaamu.

Lakini Balaamu akajibu akamwambia Balaki, Je! Sikukuambia ya kwamba, Kila neno BWANA atakalolisema sina budi kulitenda?

Balaamu akamwambia Balaki, Je! Sikuwaambia wajumbe wako ulionitumia, nikisema,

Hata Balaki angenipa nyumba yake imejaa fedha na dhahabu, siwezi kukiuka neno la BWANA, kutenda neno jema, wala neno baya, kwa nia yangu mwenyewe; BWANA atakalolinena ndilo nitakalolinena mimi.

Lakini Petro akamwambia, Fedha yako na ipotelee mbali pamoja nawe, kwa kuwa umedhania ya kuwa karama ya Mungu yapatikana kwa mali.

Wanakiri ya kwamba wanamjua Mungu, bali kwa matendo yao wanamkana; ni wenye machukizo, waasi, wala hawafai kwa tendo lolote jema.

lakini sikukubali kumsikiliza Balaamu; kwa hiyo akafululiza kuwabariki; basi nikawatoa katika mkono wake.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo