Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Hesabu 2:18 - Swahili Revised Union Version

18 Upande wa magharibi kutakuwa na bendera ya kambi ya Efraimu kwa majeshi yao; na mkuu wa wana wa Efraimu atakuwa Elishama mwana wa Amihudi.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

18 “Kwa upande wa magharibi, wale walio chini ya bendera ya kundi la Efraimu watapiga kambi kulingana na makundi yao, kiongozi wao akiwa Elishama mwana wa Amihudi,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

18 “Kwa upande wa magharibi, wale walio chini ya bendera ya kundi la Efraimu watapiga kambi kulingana na makundi yao, kiongozi wao akiwa Elishama mwana wa Amihudi,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

18 “Kwa upande wa magharibi, wale walio chini ya bendera ya kundi la Efraimu watapiga kambi kulingana na makundi yao, kiongozi wao akiwa Elishama mwana wa Amihudi,

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

18 Upande wa magharibi kutakuwa na kambi ya makundi ya Efraimu chini ya beramu yao. Kiongozi wa watu wa Efraimu ni Elishama mwana wa Amihudi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

18 Upande wa magharibi kutakuwepo na kambi ya makundi ya Efraimu chini ya alama yao. Kiongozi wa watu wa Efraimu ni Elishama mwana wa Amihudi.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

18 Upande wa magharibi kutakuwa na bendera ya kambi ya Efraimu kwa majeshi yao; na mkuu wa wana wa Efraimu atakuwa Elishama mwana wa Amihudi.

Tazama sura Nakili

Hesabu 2:18
13 Marejeleo ya Msalaba  

Basi sasa wanao wawili uliozaliwa katika nchi ya Misri kabla sijaja kwako Misri ni watoto wangu, yaani, Efraimu na Manase watakuwa wangu, kama Reubeni na Simeoni.

Watakuja kwa kulia, na kwa maombi nitawaongoza; nitawapitisha kwenye mito ya maji, katika njia iliyonyoka; katika njia hiyo hawatajikwaa; maana mimi ni baba wa Israeli, na Efraimu ni mzaliwa wa kwanza wangu.

Katika wana wa Yusufu; wa Efraimu, Elishama mwana wa Amihudi; na wa Manase; Gamalieli mwana wa Pedasuri.

Katika wana wa Yusufu, maana katika wana wa Efraimu, vizazi vyao kwa kufuata jamaa zao, na nyumba za baba zao, kama hesabu ya majina, kuanzia umri wa miaka ishirini na zaidi, wote walioweza kwenda vitani,

Kisha beramu ya kambi ya wana wa Efraimu ikasafiri kwenda mbele kwa majeshi yao; na juu ya jeshi lake ni Elishama mwana wa Amihudi.

Na jeshi lake, na wale waliohesabiwa kwao walikuwa elfu arubaini na mia tano.

Siku ya saba Elishama mwana wa Amihudi, mkuu wa wana wa Efraimu;

tena kwa ajili ya dhabihu ya sadaka za amani, ng'ombe dume wawili, na kondoo dume watano, na mbuzi dume watano, na wana-kondoo dume watano wa mwaka mmoja; hayo ndiyo matoleo ya Elishama mwana wa Amihudi.

Mzaliwa wa kwanza wa ng'ombe wake mume, enzi ni yake; Na pembe zake ni pembe za nyati; Kwa hizo atayasukuma mataifa yote, hata ncha za nchi; Nao ni makumi ya maelfu ya Efraimu, Nao ni maelfu ya Manase.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo