Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Hesabu 2:17 - Swahili Revised Union Version

17 Ndipo hema ya kukutania itasafiri, pamoja na kambi za Walawi katikati ya kambi zote; kama wapangavyo kambi, watasafiri vivyo hivyo, kila mtu mahali pake, penye bendera zao.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

17 “Halafu, kambi ya kabila la Walawi, ikiwa katikati ya kambi zote, na wakiwa wamebeba hilo hema la mkutano, wataondoka; kila kundi litasafiri kwa kufuata nafasi yake chini ya bendera yao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

17 “Halafu, kambi ya kabila la Walawi, ikiwa katikati ya kambi zote, na wakiwa wamebeba hilo hema la mkutano, wataondoka; kila kundi litasafiri kwa kufuata nafasi yake chini ya bendera yao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

17 “Halafu, kambi ya kabila la Walawi, ikiwa katikati ya kambi zote, na wakiwa wamebeba hilo hema la mkutano, wataondoka; kila kundi litasafiri kwa kufuata nafasi yake chini ya bendera yao.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

17 Kisha Hema la Kukutania na kambi ya Walawi vitakuwa katikati ya kambi zote. Wao watasafiri kwa utaratibu ule ule kama walivyopiga kambi, kila mmoja mahali pake mwenyewe chini ya beramu yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

17 Kisha Hema la Kukutania na kambi ya Walawi vitakuwa katikati ya kambi zote. Wao watasafiri kwa utaratibu ule ule kama walivyopiga kambi, kila mmoja mahali pake mwenyewe chini ya alama yake.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

17 Ndipo hema ya kukutania itasafiri, pamoja na kambi za Walawi katikati ya kambi zote; kama wapangavyo kambi, watasafiri vivyo hivyo, kila mtu mahali pake, penye bendera zao.

Tazama sura Nakili

Hesabu 2:17
8 Marejeleo ya Msalaba  

Na maskani ilishushwa; na wana wa Gershoni, na wana wa Merari, walioichukua maskani, wakasafiri kwenda mbele.

Ndipo wakasafiri Wakohathi wenye kuvichukua vile vitu vitakatifu; na hao wengine wakaisimamisha maskani kabla hawajaja wao.

BWANA akanena na Musa na Haruni, na kuwaambia,

Upande wa magharibi kutakuwa na bendera ya kambi ya Efraimu kwa majeshi yao; na mkuu wa wana wa Efraimu atakuwa Elishama mwana wa Amihudi.

Na hao watakaopanga mbele ya maskani upande wa mashariki, mbele ya hema ya kukutania upande wa kuelekea maawio ya jua, watakuwa hawa, Musa na Haruni na wanawe, wenye kulinda ulinzi wa mahali patakatifu, yaani, huo ulinzi wa wana wa Israeli; na mgeni atakayekaribia atauawa.

Lakini mambo yote na yatendeke kwa uzuri na kwa utaratibu.

Maana nijapokuwa sipo kwa mwili, lakini nipo pamoja nanyi kwa roho, nikifurahi na kuuona utaratibu wenu na uthabiti wa imani yenu katika Kristo.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo