Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Hesabu 18:12 - Swahili Revised Union Version

12 Yaliyo mazuri katika mafuta, na yaliyo mazuri ya mavuno ya zabibu, na ya mavuno ya nafaka, malimbuko yake watakayompa BWANA, hayo nimekupa wewe.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

12 “Ninakupa vitu vyote vizuri vinavyotokana na malimbuko ambayo Waisraeli hunitolea: Mafuta safi, divai na nafaka.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

12 “Ninakupa vitu vyote vizuri vinavyotokana na malimbuko ambayo Waisraeli hunitolea: Mafuta safi, divai na nafaka.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

12 “Ninakupa vitu vyote vizuri vinavyotokana na malimbuko ambayo Waisraeli hunitolea: mafuta safi, divai na nafaka.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

12 “Ninawapa mafuta ya zeituni yaliyo bora kuliko yote, na divai mpya iliyo bora kuliko zote na nafaka wanazompa Mwenyezi Mungu kama malimbuko katika mavuno yao.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

12 “Ninawapa mafuta ya zeituni yaliyo bora kuliko yote, na divai mpya iliyo bora kuliko zote na nafaka wanazompa bwana kama malimbuko katika mavuno yao.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

12 Yaliyo mazuri katika mafuta, na yaliyo mazuri ya mavuno ya zabibu, na ya mavuno ya nafaka, malimbuko yake watakayompa BWANA, hayo nimekupa wewe.

Tazama sura Nakili




Hesabu 18:12
19 Marejeleo ya Msalaba  

Mungu na akupe ya umande wa mbingu, Na manono ya nchi, Na wingi wa nafaka na mvinyo.


Tena, akaja mtu kutoka Baal-shalisha, akamletea mtu wa Mungu chakula cha malimbuko, mikate ishirini ya shayiri, na masuke mabichi ya ngano guniani. Akasema, Uwape watu, ili wale.


Mara amri ilipovavagaa, wana wa Israeli wakatoa kwa wingi malimbuko ya nafaka, divai, mafuta, asali, na mazao yote ya mashamba; na zaka za vitu vyote wakazileta kwa wingi.


Ndiye aletaye amani mipakani mwako, Hukushibisha kwa ngano safi.


Naam, ningewalisha kwa ngano iliyo bora zaidi, Ningewashibisha kwa asali itokayo mwambani.


Usikawie kuleta malimbuko ya matunda yako na ya vinywaji vyako. Mzaliwa wa kwanza katika wanao wanaume utanipa mimi.


Ya kwanza ya malimbuko ya nchi yako utayaleta na kuyatia ndani ya nyumba ya BWANA, Mungu wako. Usimtokose mwana-mbuzi katika maziwa ya mama yake.


Vitu vya kwanza vya malimbuko ya nchi yako utavileta na kuvitia ndani ya nyumba ya BWANA Mungu wako. Usimtokose mwana-mbuzi katika maziwa ya mama yake.


Na kitu cha kwanza cha malimbuko yote ya vitu vyote, na kila toleo la kila kitu cha matoleo yenu, litakuwa la makuhani. Tena mtampa kuhani sehemu ya kwanza ya unga mbichi, ili kuleta baraka juu ya nyumba yako.


Vitu hivyo mtavisongeza kwa BWANA kuwa ni malimbuko; lakini visifike juu ya madhabahu kuwa ni harufu ya kupendeza.


Nawe kwamba wamtolea BWANA sadaka ya unga ya malimbuko, utatoa hiyo ngano katika masuke yake iliyochomwa motoni, ngano iliyopondwa ya masuke mabichi, ndiyo utakayoleta kuwa sadaka ya unga ya malimbuko yako.


Mtatoa katika makao yenu mikate miwili ya kutikiswa, itakuwa ya sehemu za kumi mbili za efa; itakuwa ya unga mwembamba, itaokwa na chachu, iwe malimbuko kwa BWANA.


Kisha kuhani atawatikisa pamoja na hiyo mikate ya malimbuko kuwa sadaka ya kutikiswa mbele za BWANA, pamoja na wale wana-kondoo wawili; watakuwa watakatifu kwa BWANA, wawe wa huyo kuhani.


Na hii itakuwa haki ya makuhani kwa watu hao wasongezao sadaka, ikiwa ni ng'ombe au kondoo wampe kuhani mkono, na mashavu mawili, na tumbo.


Malimbuko ya nafaka zako, na divai yako, na mafuta yako, na manyoya ya kwanza ya kondoo wako, umpe.


twaa malimbuko ya ardhi, utakayoyavuna katika nchi akupayo BWANA, Mungu wako; ukayatie katika kikapu, ukaende hata mahali pale atakapopachagua BWANA, Mungu wako, ili alikalishe jina lake huko.


Siagi ya ng'ombe, na maziwa ya kondoo, Pamoja na mafuta ya wana-kondoo, Kondoo dume wa Kibashani, na mbuzi, Na unono wa ngano iliyo nzuri; Ukanywa divai, damu ya mizabibu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo