Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Hesabu 18:11 - Swahili Revised Union Version

11 Tena kitu hiki ni chako; ile sadaka ya kuinuliwa ya kipawa chao, maana, sadaka za kutikiswa zote za wana wa Israeli; hizi nimekupa wewe, na wanao na binti zako pamoja nawe, ni haki yenu milele; kila mtu katika nyumba yako aliye safi atakula katika hizo.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 “Pia, vitu vingine vyote watakavyonitolea Waisraeli kama sadaka za kutikisa, vitakuwa vyako. Ninakupa wewe, wanao na binti zako kuwa haki yenu milele. Mtu yeyote katika jamaa yako asiye najisi anaweza kula vitu hivyo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 “Pia, vitu vingine vyote watakavyonitolea Waisraeli kama sadaka za kutikisa, vitakuwa vyako. Ninakupa wewe, wanao na binti zako kuwa haki yenu milele. Mtu yeyote katika jamaa yako asiye najisi anaweza kula vitu hivyo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 “Pia, vitu vingine vyote watakavyonitolea Waisraeli kama sadaka za kutikisa, vitakuwa vyako. Ninakupa wewe, wanao na binti zako kuwa haki yenu milele. Mtu yeyote katika jamaa yako asiye najisi anaweza kula vitu hivyo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 “Hiki pia ni chako: chochote kilichotengwa kutoka matoleo yote ya sadaka za kuinuliwa za Waisraeli. Haya ninakupa wewe, na wanao wa kiume na wa kike kuwa sehemu yenu ya milele. Kila mmoja wa nyumba yako ambaye ametakasika anaweza kuyala.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 “Hiki pia ni chako: chochote kilichotengwa kutoka kwenye matoleo yote ya sadaka za kuinuliwa za Waisraeli. Ninakupa wewe haya, wana na binti zako kama sehemu yenu ya kawaida. Kila mmoja wa nyumba yako ambaye ni safi kwa taratibu za ibada anaweza kuyala.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

11 Tena kitu hiki ni chako; ile sadaka ya kuinuliwa ya kipawa chao, maana, sadaka za kutikiswa zote za wana wa Israeli; hizi nimekupa wewe, na wanao na binti zako pamoja nawe, ni haki yenu milele; kila mtu katika nyumba yako aliye safi atakula katika hizo.

Tazama sura Nakili

Hesabu 18:11
10 Marejeleo ya Msalaba  

Na kidari cha kutikiswa, na mguu wa kuinuliwa, mtavila katika mahali palipo safi; wewe, na wanao, na binti zako pamoja nawe; kwa maana vimetolewa kuwa ni haki yako, na haki ya wanao, katika zile kafara za sadaka za amani za wana wa Israeli.

Na katika hayo atasongeza kimoja katika kila toleo kiwe sadaka ya kuinuliwa kwa BWANA; itakuwa ni ya kuhani atakayeinyunyiza hiyo damu ya sadaka za amani.

BWANA akamwambia Haruni, Wewe na wanao na nyumba ya baba zako pamoja nawe mtachukua uovu wa patakatifu; wewe na wanao pamoja nawe mtauchukua ukuhani wenu.

Utakula vitu hivyo kuwa ni vitu vitakatifu sana; kila mwanamume atakula vitu hivyo; vitakuwa vitakatifu kwako wewe.

Sadaka zote za kuinuliwa za vitu vitakatifu, wana wa Israeli wavisongezavyo kwa BWANA, nimekupa wewe na wanao na binti zako pamoja nawe, ni haki yenu ya milele; ni agano la chumvi la milele mbele za BWANA kwa ajili yako, na kizazi chako pamoja nawe.

Kisha BWANA akamwambia Haruni, Tazama, nimekupa wewe ulinzi wa sadaka zangu za kuinuliwa, maana, vitu vyote vya hao wana wa Israeli vilivyowekwa wakfu; nimekupa wewe na wanao vitu hivyo kwa ajili ya kule kutiwa mafuta kwenu, kuwa haki yenu milele.

Na hii itakuwa haki ya makuhani kwa watu hao wasongezao sadaka, ikiwa ni ng'ombe au kondoo wampe kuhani mkono, na mashavu mawili, na tumbo.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo