Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Hesabu 14:27 - Swahili Revised Union Version

27 Je! Nivumilie na mkutano mwovu huu uninung'unikiao hadi lini? Nimesikia manung'uniko ya wana wa Israeli, waninung'unikiayo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

27 “Kundi hili la watu waovu litaendelea kuninungunikia mpaka lini? Nimechoka na haya manunguniko ya Waisraeli juu yangu!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

27 “Kundi hili la watu waovu litaendelea kuninungunikia mpaka lini? Nimechoka na haya manunguniko ya Waisraeli juu yangu!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

27 “Kundi hili la watu waovu litaendelea kuninung'unikia mpaka lini? Nimechoka na haya manung'uniko ya Waisraeli juu yangu!

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

27 “Jumuiya hii ovu itanung’unika dhidi yangu hadi lini? Nimesikia malalamiko ya hawa Waisraeli wanaonung’unika.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

27 “Jumuiya hii ovu itanung’unika dhidi yangu hadi lini? Nimesikia malalamiko ya hawa Waisraeli wanaonung’unika.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

27 Je! Nivumilie na mkutano mwovu huu uninung'unikiao hadi lini? Nimesikia manung'uniko ya wana wa Israeli, waninung'unikiayo.

Tazama sura Nakili




Hesabu 14:27
11 Marejeleo ya Msalaba  

Nimeyasikia manung'uniko ya wana wa Israeli; haya sema nao ukinena, Wakati wa jioni mtakula nyama, na wakati wa asubuhi mtashiba mkate; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.


BWANA akamwambia Musa, Mtakataa kuyashika maagizo yangu na sheria zangu hata lini?


na asubuhi ndipo mtakapouona utukufu wa BWANA; kwa kuwa yeye husikia manung'uniko yenu mliyomnung'unikia BWANA; na sisi tu nani, hata mkatunung'unikia?


Musa akamwambia Haruni, Haya, sema na mkutano wote wa wana wa Israeli, Njoni karibu mbele ya BWANA; kwa kuwa yeye ameyasikia manung'uniko yenu.


Nanyi mmejitukuza juu yangu kwa vinywa vyenu, na kuyaongeza maneno juu yangu; nimesikia mimi.


Kisha hao watu walikuwa kama wanung'unikao, wakinena maovu masikioni mwa BWANA; BWANA aliposikia hayo, hasira zake zikawaka; na moto wa BWANA ukawaka kati yao, ukateketeza hadi viunga vya kambi.


BWANA akamwuliza Musa, Je! Watu hawa watanidharau hadi lini? Wasiniamini hadi lini? Nijapokuwa nimefanya ishara hizo zote kati yao.


Kisha BWANA akanena na Musa na Haruni, na kuwaambia,


Yesu akaja, akawagusa, akasema, Inukeni, wala msiogope.


Akawajibu, akasema, Enyi kizazi kisichoamini, nikae nanyi hadi lini? Nichukuliane nanyi hadi lini? Mleteni kwangu.


Wala msinung'unike, kama wengine wao walivyonung'unika, wakauawa na mharibifu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo