Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Danieli 2:35 - Swahili Revised Union Version

35 Ndipo kile chuma, na ule udongo, na ile shaba, na ile fedha, na ile dhahabu, vilivunjwa vipande vipande pamoja vikawa kama makapi ya viwanja vya kupepetea wakati wa joto; upepo ukavipeperusha hata pasionekane mahali pake; na lile jiwe lililoipiga hiyo sanamu likawa milima mikubwa, likaijaza dunia yote.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

35 Mara kile chuma, udongo wa mfinyanzi, shaba, fedha na dhahabu, vyote vikavunjika vipandevipande na kuwa kama makapi ya mahali pa kupuria nafaka wakati wa kiangazi. Upepo ukavipeperushia mbali kisibakie hata kipande kimoja. Lakini lile jiwe lililoivunja ile sanamu likageuka kuwa mlima mkubwa na kuijaza dunia yote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

35 Mara kile chuma, udongo wa mfinyanzi, shaba, fedha na dhahabu, vyote vikavunjika vipandevipande na kuwa kama makapi ya mahali pa kupuria nafaka wakati wa kiangazi. Upepo ukavipeperushia mbali kisibakie hata kipande kimoja. Lakini lile jiwe lililoivunja ile sanamu likageuka kuwa mlima mkubwa na kuijaza dunia yote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

35 Mara kile chuma, udongo wa mfinyanzi, shaba, fedha na dhahabu, vyote vikavunjika vipandevipande na kuwa kama makapi ya mahali pa kupuria nafaka wakati wa kiangazi. Upepo ukavipeperushia mbali kisibakie hata kipande kimoja. Lakini lile jiwe lililoivunja ile sanamu likageuka kuwa mlima mkubwa na kuijaza dunia yote.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

35 Ndipo ile chuma, ule udongo, ile shaba, ile fedha na ile dhahabu vikavunjika vipande vipande kwa wakati mmoja, na vikawa kama makapi katika sakafu ya kupuria nafaka wakati wa kiangazi. Upepo ukavipeperusha bila kuacha hata alama. Lakini lile jiwe lililoipiga ile sanamu likawa mlima mkubwa mno na kuijaza dunia yote.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

35 Ndipo ile chuma, ule udongo wa mfinyanzi, ile shaba, ile fedha na ile dhahabu vikavunjika vipande vipande kwa wakati mmoja, na vikawa kama makapi katika sakafu ya kupuria nafaka wakati wa kiangazi. Upepo ukavipeperusha bila kuacha hata alama. Lakini lile jiwe lililoipiga ile sanamu likawa mlima mkubwa mno na kuijaza dunia yote.

Tazama sura Nakili

Swahili Roehl Bible 1937

35 Ndipo, yote pia yalipopondeka kwa mara moja, chuma, udongo, shaba, fedha, dhahabu, yakawa kama makapi penye kupuria ngano siku za kiangazi, upepo ukayapeperusha, yakatoweka kabisa, hata mahali pao hapakujulika. Lakini lile jiwe lililokiponda kile kinyago likawa mlima mkubwa, ukaieneza nchi yote.

Tazama sura Nakili




Danieli 2:35
28 Marejeleo ya Msalaba  

Wakati vipatapo moto hutoweka; Kukiwako joto, hukoma mahali pao.


Maana upepo hupita juu yake, na kutoweka! Lisionekane mahali lilipokuwa tena.


Miisho yote ya dunia itakumbuka, Na watu watamrejea BWANA; Jamaa zote za mataifa watamsujudia.


Maana bado kitambo kidogo asiye haki hatakuwapo, Utapaangalia mahali pake wala hatakuwapo.


Nikapita na kumbe! Hayuko, Nikamtafuta wala hakuonekana.


Avikomesha vita hata mwisho wa dunia; Avunja uta, akata mkuki, achoma moto magari.


Nchi yote itakusujudia na kukuimbia, Naam, italiimbia jina lako.


Mataifa yote uliyoyaumba watakuja; Watakusujudia Wewe, Bwana, Watalitukuza jina lako;


Hawatadhuru wala hawataharibu katika mlima wangu wote mtakatifu; maana dunia itajawa na kumjua BWANA, kama vile maji yanavyoifunika bahari.


Ungameni pamoja, enyi makabila ya watu, Nanyi mtavunjwa vipande vipande; Tegeni masikio, ninyi nyote wa nchi zilizo mbali; Jitahidini, nanyi mtavunjwa vipande vipande; Jitahidini, nanyi mtavunjwa vipande vipande.


Na katika siku za wafalme hao Mungu wa mbinguni atausimamisha ufalme ambao hautaangamizwa milele, wala watu wengine hawataachiwa enzi yake; bali utavunja falme hizi zote vipande vipande na kuziharibu, nao utasimama milele na milele.


Kwa sababu hiyo watakuwa kama wingu la asubuhi, na kama umande utowekao upesi, kama makapi yaliyopeperushwa na tufani sakafuni, na kama moshi utokao katika bomba.


Haya, simama upure, Ee binti Sayuni; kwa maana nitafanya pembe yako kuwa chuma, na kwato zako kuwa shaba; nawe utapondaponda mataifa mengi, na faida yao utaiweka wakfu kwa BWANA, na mali zao kwa BWANA wa dunia yote.


Tena itakuwa siku hiyo, nitafanya Yerusalemu kuwa jiwe la kuwalemea watu wa kabila zote; wote watakaojitwika jiwe hilo watapata majeraha mengi; na mataifa yote ya dunia watakusanyika pamoja juu yake.


Maana sharti amiliki yeye, hata awaweke adui zake wote chini ya miguu yake.


Malaika wa saba akapiga baragumu, pakawa na sauti kuu katika mbingu, zikisema, Ufalme wa dunia umekwisha kuwa ufalme wa Bwana wetu na wa Kristo wake, naye atamiliki hata milele na milele.


lakini hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni.


Kisha nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, na yeye aketiye juu yake; ambaye nchi na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo