Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Danieli 2:34 - Swahili Revised Union Version

34 Nawe ukatazama hata jiwe likachongwa bila kazi ya mikono, nalo jiwe hilo likaipiga sanamu miguu yake, iliyokuwa ya chuma na udongo, likaivunja vipande vipande.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

34 Ukiwa bado unaangalia, jiwe lilingoka lenyewe, bila kuguswa, na kuipondaponda miguu ya shaba na udongo wa mfinyanzi ya ile sanamu, na kuivunja vipandevipande.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

34 Ukiwa bado unaangalia, jiwe lilingoka lenyewe, bila kuguswa, na kuipondaponda miguu ya shaba na udongo wa mfinyanzi ya ile sanamu, na kuivunja vipandevipande.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

34 Ukiwa bado unaangalia, jiwe liling'oka lenyewe, bila kuguswa, na kuipondaponda miguu ya shaba na udongo wa mfinyanzi ya ile sanamu, na kuivunja vipandevipande.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

34 Ulipokuwa unaangalia, jiwe lilikatwa, lakini si kwa mikono ya mwanadamu. Lile jiwe liliipiga ile sanamu kwenye nyayo zake za chuma na udongo, na kuivunja.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

34 Ulipokuwa unaangalia, jiwe lilikatwa, lakini si kwa mikono ya mwanadamu. Lile jiwe liliipiga ile sanamu kwenye nyayo zake za chuma na udongo wa mfinyanzi, na kuivunja.

Tazama sura Nakili

Swahili Roehl Bible 1937

34 Ulipokuwa unakitazama, mara jiwe likaporomoka lenyewe lisilotupwa na mikono ya watu, likakipiga kile kinyago penye miguu yake iliyokuwa ya chuma na ya udongo, likaiponda.

Tazama sura Nakili




Danieli 2:34
25 Marejeleo ya Msalaba  

Jiwe walilolikataa waashi Limekuwa jiwe kuu la pembeni.


kwa ajili ya hayo Bwana, MUNGU, asema hivi, Tazama, naweka jiwe katika Sayuni, liwe msingi, jiwe lililojaribiwa, jiwe la pembeni lenye thamani, msingi ulio imara; yeye aaminiye hatafanya haraka.


Kwa maana kila taifa na ufalme wa watu Wasiotaka kukutumikia wataangamia; Naam, mataifa hayo wataharibiwa kabisa.


Ungameni pamoja, enyi makabila ya watu, Nanyi mtavunjwa vipande vipande; Tegeni masikio, ninyi nyote wa nchi zilizo mbali; Jitahidini, nanyi mtavunjwa vipande vipande; Jitahidini, nanyi mtavunjwa vipande vipande.


Lakini utavunjika kati ya hao wasiotahiriwa, nawe utalala pamoja nao waliouawa kwa upanga.


Kisha akapima dhiraa elfu moja, yakawa mto nisioweza kuuvuka; maana maji yamezidi, maji ya kuogelea, mto usiovukika.


miguu yake ni ya chuma; na nyayo za miguu yake nusu ya chuma na nusu ya udongo.


Na ufalme, na mamlaka, na ukuu wa ufalme, chini ya mbingu zote, watapewa watu wa watakatifu wake Aliye Juu; ufalme wake ni ufalme wa milele, na wote wenye mamlaka watamtumikia na kumtii.


Na kwa mashauri yake atafanikisha hila mkononi mwake; naye atajitukuza nafsi yake moyoni mwake; naye atawaangamiza wengi katika hali yao ya salama; naye atasimama kushindana naye aliye Mkuu wa wakuu; lakini atavunjika, bila kazi ya mikono.


Tena itakuwa siku hiyo, nitafanya Yerusalemu kuwa jiwe la kuwalemea watu wa kabila zote; wote watakaojitwika jiwe hilo watapata majeraha mengi; na mataifa yote ya dunia watakusanyika pamoja juu yake.


Akajibu akaniambia, akisema, Hili ndilo neno la BWANA kwa Zerubabeli, kusema, Si kwa uwezo, wala si kwa nguvu, bali ni kwa roho yangu, asema BWANA wa majeshi.


Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.


waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu.


Yeye ndiye jiwe lile lililodharauliwa na ninyi waashi, nalo limewekwa kuwa jiwe kuu la pembeni.


Kwa maana twajua ya kuwa nyumba ya maskani yetu iliyo ya dunia hii ikiharibiwa, tunalo jengo litokalo kwa Mungu, nyumba isiyofanywa kwa mikono, iliyo ya milele mbinguni.


Kwa sababu Kristo hakuingia katika patakatifu palipofanyika kwa mikono, ndio mfano wa patakatifu halisi; bali aliingia mbinguni hasa, aonekane sasa usoni pa Mungu kwa ajili yetu;


Basi, heshima hii ni kwenu ninyi mnaoamini. Bali kwao wasioamini, Jiwe walilolikataa waashi, Limekuwa jiwe kuu la pembeni.


Malaika wa saba akapiga baragumu, pakawa na sauti kuu katika mbingu, zikisema, Ufalme wa dunia umekwisha kuwa ufalme wa Bwana wetu na wa Kristo wake, naye atamiliki hata milele na milele.


Hawa watafanya vita na Mwana-kondoo, na Mwana-kondoo atawashinda, kwa maana Yeye ni Bwana wa Mabwana, na Mfalme wa Wafalme, na hao walio pamoja naye ndio walioitwa, na wateule, na waaminifu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo