Danieli 11:4 - Swahili Revised Union Version4 Naye atakaposimama, ufalme wake utavunjika, na kugawanyika katika pepo nne za mbinguni; lakini hautakuwa wa uzao wake, wala hautakuwa kama mamlaka yake ambayo alitawala kwayo; kwa maana ufalme wake utang'olewa, hata kwa ajili ya wengine zaidi ya hao. Tazama suraMatoleo zaidiBiblia Habari Njema4 Hata hivyo, wakati wa kilele cha uwezo wake, ufalme wake utavunjika na kugawanyika katika sehemu nne kuelekea pepo nne za mbingu. Wazawa wake hawatatawala, wala ufalme hautakuwa mikononi mwa milki aliyotawala, kwa sababu ufalme wake utachukuliwa na wengine. Tazama suraBiblia Habari Njema - BHND4 Hata hivyo, wakati wa kilele cha uwezo wake, ufalme wake utavunjika na kugawanyika katika sehemu nne kuelekea pepo nne za mbingu. Wazawa wake hawatatawala, wala ufalme hautakuwa mikononi mwa milki aliyotawala, kwa sababu ufalme wake utachukuliwa na wengine. Tazama suraBiblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza4 Hata hivyo, wakati wa kilele cha uwezo wake, ufalme wake utavunjika na kugawanyika katika sehemu nne kuelekea pepo nne za mbingu. Wazawa wake hawatatawala, wala ufalme hautakuwa mikononi mwa milki aliyotawala, kwa sababu ufalme wake utachukuliwa na wengine. Tazama suraNeno: Bibilia Takatifu4 Baada ya kujitokeza, himaya yake itavunjwa na kugawanyika katika pande nne za mbinguni. Hautaenda kwa wazao wake, wala hautakuwa na nguvu alizokuwa nazo, kwa sababu himaya yake itang’olewa na kupewa wengine. Tazama suraNeno: Maandiko Matakatifu4 Baada ya kujitokeza, milki yake itavunjwa na kugawanyika katika pande nne za mbinguni. Hautakwenda kwa wazao wake, wala hautakuwa na nguvu alizotumia, kwa sababu milki yake itang’olewa na kupewa wengine. Tazama suraSwahili Roehl Bible 19374 Lakini hapo, atakapokwisha kuondokea, ufalme wake utavunjika, ukatwe vipande kwenye pepo zote nne za mbinguni; lakini hautakuwa wao walio uzao wake, wala hapatakuwa atakayetawala, kama yeye alivyotawala, kwani ufalme wake utang'olewa, uwe wa wengine, wale wasiupate. Tazama sura |