Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Danieli 10:6 - Swahili Revised Union Version

6 mwili wake pia ulikuwa kama zabarajadi safi, na uso wake mfano wa umeme, na macho yake kama taa za moto, na mikono yake na miguu yake rangi yake kama shaba iliyosuguliwa sana, na sauti ya maneno yake kama sauti ya umati wa watu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

6 Mwili wake ulingaa kama zabarajadi safi. Uso wake ulifanana na umeme, na macho yake yaliwaka kama miali ya moto. Miguu na mikono yake ilingaa kama shaba iliyosuguliwa sana. Sauti yake ilivuma kama sauti ya umati mkubwa wa watu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

6 Mwili wake ulingaa kama zabarajadi safi. Uso wake ulifanana na umeme, na macho yake yaliwaka kama miali ya moto. Miguu na mikono yake ilingaa kama shaba iliyosuguliwa sana. Sauti yake ilivuma kama sauti ya umati mkubwa wa watu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

6 Mwili wake uling'aa kama zabarajadi safi. Uso wake ulifanana na umeme, na macho yake yaliwaka kama miali ya moto. Miguu na mikono yake iling'aa kama shaba iliyosuguliwa sana. Sauti yake ilivuma kama sauti ya umati mkubwa wa watu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

6 Mwili wake ulikuwa kama zabarajadi safi, uso wake kama radi, macho yake kama miali wa moto, mikono yake na miguu yake kama mng’ao wa shaba iliyosuguliwa, nayo sauti yake kama ya umati mkubwa wa watu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

6 Mwili wake ulikuwa kama kito cha zabarajadi safi, uso wake kama umeme wa radi, macho yake kama mwali wa moto, mikono yake na miguu yake kama mng’ao wa shaba iliyosuguliwa sana, nayo sauti yake kama ya umati mkubwa wa watu.

Tazama sura Nakili

Swahili Roehl Bible 1937

6 Mwili wake ulikuwa kama kito cha Tarsisi, uso wake ulionekana kuwa kama umeme, nayo macho yake yalikuwa kama mienge ya moto, mikono yake na miguu yake ilimerimeta kama shaba iliyokatuliwa, sauti ya kusema kwake ikawa kama uvumi wa watu wengi.

Tazama sura Nakili




Danieli 10:6
18 Marejeleo ya Msalaba  

na safu ya nne itakuwa ni zabarajadi, shohamu na yaspi; vito hivyo vitakazwa ndani ya dhahabu kwa kujaa mahali pake.


Mikono yake ni kama mianzi ya dhahabu, lliyopambwa kwa zabarajadi; Kiwiliwili chake kama kazi ya pembe, Iliyonakishiwa kwa yakuti samawi;


Na wale viumbe hai walipiga mbio, kwenda na kurudi, kama kuonekana kwa kumulika kwa umeme.


Kuonekana kwake magurudumu hayo na kazi yake kulikuwa kama rangi ya zabarajadi; nayo yote manne yalikuwa na mfano mmoja; na kuonekana kwake na kazi yake kulikuwa kana kwamba ni gurudumu ndani ya gurudumu lingine.


Nao walipokwenda nilisikia mshindo wa mabawa yao, kama mshindo wa maji makuu, kama sauti yake Mwenyezi, mshindo wa mvumo, kama mshindo wa jeshi; hapo waliposimama walishusha mabawa yao.


Na miguu yao ilikuwa miguu iliyonyoka; na nyayo za miguu yao zilikuwa kama nyayo za miguu ya ndama; zikimetameta kama rangi ya shaba iliyosuguliwa sana.


Nami nikaangalia, na tazama, yalikuwako magurudumu manne karibu na makerubi, gurudumu moja karibu na kerubi mmoja, na gurudumu lingine karibu na kerubi mwingine; na kuonekana kwa magurudumu kulikuwa kana kwamba ni zabarajadi.


Akanileta huko, na tazama, alikuwapo mtu, ambaye kuonekana kwake kulikuwa kama kuonekana kwa shaba, naye alikuwa na uzi wa kitani mkononi mwake, na mwanzi wa kupimia; akasimama karibu na lango.


Ndipo nikaangalia, na tazama, palikuwa na kitu kilichofanana na mwanadamu; kuanzia kilichoonekana kama viuno vyake kwenda chini ilikuwa moto; na kuanzia kilichoonekana kama viuno vyake kwenda juu, ilikuwa mfano wa mwangaza, kama rangi ya kaharabu.


akageuka sura yake mbele yao; uso wake ukang'aa kama jua, mavazi yake yakawa meupe kama nuru.


Na sura yake ilikuwa kama umeme, na mavazi yake meupe kama theluji.


Ikawa katika kusali kwake sura ya uso wake ikageuka, mavazi yake yakawa meupe, yakimetameta.


Kisha nikaona malaika mwingine mwenye nguvu akishuka kutoka mbinguni, amevikwa wingu; na upinde wa mvua juu ya kichwa chake; na uso wake ulikuwa kama jua, na miguu yake kama nguzo za moto.


Na macho yake yalikuwa kama muali wa moto, na juu ya kichwa chake vilemba vingi; naye ana jina lililoandikwa, asilolijua mtu ila yeye mwenyewe.


Na kwa malaika wa kanisa lililoko Thiatira andika; Haya ndiyo anenayo Mwana wa Mungu, yeye aliye na macho yake kama muali wa moto, na miguu yake mfano wa shaba iliyosuguliwa sana.


wa tano sardoniki; wa sita akiki; wa saba krisolitho; wa nane zabarajadi; wa tisa yakuti ya manjano; wa kumi krisopraso; wa kumi na moja hiakintho; wa kumi na mbili amethisto.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo