Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Danieli 1:10 - Swahili Revised Union Version

10 Mkuu wa matowashi akamwambia Danieli, Mimi namwogopa bwana wangu, mfalme, aliyewaagizia ninyi chakula chenu na kinywaji chenu; kwa nini azione nyuso zenu kuwa hazipendezi kama nyuso za vijana wa rika lenu? Basi kwa kufanya hivyo mtahatarisha kichwa changu mbele ya mfalme.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

10 Lakini, towashi mkuu akamwambia Danieli, “Nina hofu kwamba bwana wangu mfalme ambaye ametoa maagizo kuhusu chakula na vinywaji unavyopaswa kutumia, ataona kuwa afya yako si nzuri kama ya wenzako wa rika lako. Hivyo maisha yangu yatakuwa hatarini.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

10 Lakini, towashi mkuu akamwambia Danieli, “Nina hofu kwamba bwana wangu mfalme ambaye ametoa maagizo kuhusu chakula na vinywaji unavyopaswa kutumia, ataona kuwa afya yako si nzuri kama ya wenzako wa rika lako. Hivyo maisha yangu yatakuwa hatarini.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

10 Lakini huyo mkuu wa maafisa akamwambia Danieli, “Ninamwogopa bwana wangu mfalme, aliyeagizia chakula na kinywaji chenu. Kwa nini aone nyuso zenu zikiwa mbaya kuliko za vijana wengine wa rika lenu? Mfalme atakata kichwa changu kwa sababu yenu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

10 lakini huyo mkuu wa maafisa akamwambia Danieli, “Ninamwogopa bwana wangu mfalme, aliyeagizia chakula na kinywaji chenu. Kwa nini aone nyuso zenu zikiwa mbaya kuliko za vijana wengine wa rika lenu? Mfalme atakata kichwa changu kwa sababu yenu.”

Tazama sura Nakili

Swahili Roehl Bible 1937

10 Naye mkuu wa watumishi wa nyumbani akamjibu Danieli: Mimi ninamwogopa bwana wangu mfalme, aniagiziaye vilaji na vinywaji vyenu; kama angewaona ninyi, ya kuwa nyuso zenu zinanuna kuliko zao vijana wengine walio rika moja nanyi, basi, mtakuwa mmeniponza kwake mfalme, akanikata kichwa.

Tazama sura Nakili

Danieli 1:10
5 Marejeleo ya Msalaba  

Kuwaogopa wanadamu huleta mtego; Bali amtumainiye BWANA atakuwa salama.

Ndipo Danieli akamwambia yule msimamizi, ambaye mkuu wa matowashi amemweka juu ya Danieli, na Hanania, na Mishaeli, na Azaria,

Basi Mungu alimjalia Danieli kupata kibali na huruma machoni pa huyo mkuu wa matowashi.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo