Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

2 Wafalme 3:11 - Swahili Revised Union Version

11 Lakini Yehoshafati akasema, Je! Hakuna nabii yeyote hapa wa BWANA ili tumwulize yeye shauri la BWANA? Akajibu mtumishi mmoja wa mfalme wa Israeli, akasema, Yupo hapa Elisha mwana wa Shafati, aliyekuwa akimimina maji juu ya mikono yake Eliya.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 Mfalme Yehoshafati akauliza, “Je, hakuna nabii yeyote hapa wa Mwenyezi-Mungu ambaye tunaweza kumwuliza shauri la Mwenyezi-Mungu?” Mtumishi mmoja wa mfalme Yoramu wa Israeli akajibu, “Elisha mwana wa Shafati yupo hapa. Yeye alikuwa mtumishi wa Elia.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 Mfalme Yehoshafati akauliza, “Je, hakuna nabii yeyote hapa wa Mwenyezi-Mungu ambaye tunaweza kumwuliza shauri la Mwenyezi-Mungu?” Mtumishi mmoja wa mfalme Yoramu wa Israeli akajibu, “Elisha mwana wa Shafati yupo hapa. Yeye alikuwa mtumishi wa Elia.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 Lakini Yehoshafati akauliza, “Je, hayuko nabii wa Mwenyezi Mungu hapa, ili tuweze kumuuliza Mwenyezi Mungu kupitia kwake?” Afisa mmoja wa mfalme wa Israeli akajibu, “Al-Yasa mwana wa Shafati yuko hapa. Ndiye alikuwa akimimina maji juu ya mikono ya Ilya.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 Lakini Yehoshafati akauliza, “Je, hayuko nabii wa bwana hapa, ili tuweze kumuuliza bwana kupitia kwake?” Afisa mmoja wa mfalme wa Israeli akajibu, “Al-Yasa mwana wa Shafati yuko hapa. Ndiye alikuwa akimimina maji juu ya mikono ya Ilya.”

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

11 Lakini Yehoshafati akasema, Je! Hakuna nabii yeyote hapa wa BWANA ili tumwulize yeye shauri la BWANA? Akajibu mtumishi mmoja wa mfalme wa Israeli, akasema, Yupo hapa Elisha mwana wa Shafati, aliyekuwa akimimina maji juu ya mikono yake Eliya.

Tazama sura Nakili

2 Wafalme 3:11
27 Marejeleo ya Msalaba  

Na yaletwe basi maji kidogo mkanawe miguu, mkapumzike chini ya mti huu.

Akarudi akiacha kumfuata, akatwaa lile jozi la ng'ombe, akawachinja, akatokosa nyama zao kwa ile miti ya ng'ombe, akawapa watu, wakala. Kisha akainuka, akamfuata Eliya, akamhudumia.

Lakini Yehoshafati akasema, Je! Hayupo hapa nabii mwingine wa BWANA, ili tumwulize yeye?

Akatoka huko akaenda mlima wa Karmeli, na toka huko akarudi mpaka Samaria.

Mfalme wa Israeli akasema, Ole wetu! Kwani BWANA amewakutanisha hawa wafalme watatu, awaue mkononi mwa Moabu.

Yehoshafati akasema, Neno la BWANA analo huyu. Basi mfalme wa Israeli, na Yehoshafati, na mfalme wa Edomu, wakamshukia.

Pamoja na hayo alishikamana na dhambi za Yeroboamu mwana wa Nebati, ambazo kwa hizo aliwakosesha Israeli; wala hakuziacha.

Basi Sauli alikufa kwa sababu ya kosa lake alilomkosa BWANA, kwa sababu ya neno la BWANA, asilolishika; na tena kwa kutaka shauri kwa mwenye pepo wa utambuzi, aulize kwake,

Daudi akamwuliza Mungu, akisema, Je! Nipande juu ya Wafilisti! Utawatia mikononi mwangu? Naye BWANA akamwambia, Panda; kwa kuwa nitawatia mikononi mwako.

Na Daudi akamwuliza Mungu tena; naye Mungu akamwambia, Hutapanda kuwafuata; zunguka mbali nao, na kuwajia ukielekea miforsadi.

Kwa kuwa ninyi hamkulichukua safari ya kwanza, BWANA, Mungu wetu, alitufurikia, kwa maana hatukumtafuta kulingana na sheria.

Lakini Yehoshafati akasema, Je! Hayupo hapa nabii mwingine wa BWANA, ili tumwulize yeye?

Hatuzioni ishara zetu, wala sasa hakuna nabii, Wala kwetu hakuna ajuaye, hadi lini?

ndipo Sedekia, mfalme, akatuma watu wamlete; naye mfalme akamwuliza kwa siri ndani ya nyumba yake, akasema, Je! Liko neno lililotoka kwa BWANA? Yeremia akasema, Liko. Akasema pia, Utatiwa katika mikono ya mfalme wa Babeli.

Hakika Bwana MUNGU hatafanya neno lolote, bila kuwafunulia watumishi wake manabii siri yake.

Ila mwajua sifa yake, ya kuwa ametumika pamoja nami kwa ajili ya Injili, kama mwana na baba yake.

na awe ameshuhudiwa kwa matendo mema; katika kulea watoto, kuwa mkaribishaji, kuwaosha watakatifu miguu, kuwasaidia wateswao, na kujitolea kutenda wema katika hali zote.

Baada ya kufa kwake Musa, mtumishi wa BWANA, BWANA akamwambia Yoshua, mwana wa Nuni, mtumishi wa Musa, akasema,

Basi wakuu hao wakatwaa katika vyakula vyao, wala wasitake shauri kinywani mwa BWANA.

Basi wana wa Israeli wakainuka, wakakwea kwenda Betheli, nao wakataka shauri kwa Mungu; wakasema, Ni nani atakayekwea kwenda vitani kwanza kwa ajili yetu juu ya wana wa Benyamini? BWANA akawaambia, Yuda atakwea kwanza.

Wana wa Israeli wakakwea juu na kulia mbele za BWANA hadi jioni; wakamwuliza BWANA, wakisema, Je! Niende nikaribie tena kupiga vita juu ya wana wa Benyamini ndugu yangu? BWANA akasema, Haya, kweeni, mwende kupigana naye.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo