Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

2 Samueli 6:12 - Swahili Revised Union Version

12 Kisha mfalme Daudi akaambiwa ya kwamba, BWANA ameibariki nyumba ya Obed-edomu, na vitu vyote alivyo navyo kwa ajili ya sanduku la Mungu. Daudi akaenda, akalileta sanduku la Mungu, toka nyumba ya Obed-edomu mpaka mji wa Daudi, kwa shangwe.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

12 Mfalme Daudi aliposikia kuwa Mwenyezi-Mungu ameibariki jamaa ya Obed-edomu na vitu vyote alivyokuwa navyo kwa sababu ya sanduku la Mungu, akaenda kulichukua sanduku la agano kutoka nyumbani kwa Obed-edomu na kulipeleka kwenye mji wa Daudi kwa shangwe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

12 Mfalme Daudi aliposikia kuwa Mwenyezi-Mungu ameibariki jamaa ya Obed-edomu na vitu vyote alivyokuwa navyo kwa sababu ya sanduku la Mungu, akaenda kulichukua sanduku la agano kutoka nyumbani kwa Obed-edomu na kulipeleka kwenye mji wa Daudi kwa shangwe.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

12 Kisha Mfalme Daudi akaambiwa, “Mwenyezi Mungu ameibariki nyumba ya Obed-Edomu pamoja na kila alicho nacho, kwa sababu ya Sanduku la Mungu.” Basi Daudi akateremka na kulipandisha Sanduku la Mungu kutoka nyumba ya Obed-Edomu hadi Mji wa Daudi kwa shangwe.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

12 Kisha Mfalme Daudi akaambiwa, “bwana ameibariki nyumba ya Obed-Edomu pamoja na kila alicho nacho, kwa sababu ya Sanduku la Mungu.” Basi Daudi akateremka na kulipandisha Sanduku la Mungu kutoka nyumba ya Obed-Edomu hadi Mji wa Daudi kwa shangwe.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

12 Kisha mfalme Daudi akaambiwa ya kwamba, BWANA ameibariki nyumba ya Obed-edomu, na vitu vyote alivyo navyo kwa ajili ya sanduku la Mungu. Daudi akaenda, akalileta sanduku la Mungu, toka nyumba ya Obed-edomu mpaka mji wa Daudi, kwa shangwe.

Tazama sura Nakili

2 Samueli 6:12
16 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini Daudi aliiteka ngome ya Sayuni; huu ndio mji wa Daudi.

Ndipo Sulemani alipowakusanya wazee wa Israeli, na wakuu wote wa makabila na wakuu wa koo za wana wa Israeli, wamwendee mfalme Sulemani huko Yerusalemu, ili walipandishe sanduku la Agano la BWANA kutoka mji wa Daudi, yaani, Sayuni.

Wazee wote wa Israeli wakaja, nao makuhani wakajitwika sanduku.

Wakalipandisha sanduku la BWANA, na ile hema ya kukutania, na vyombo vitakatifu vyote vilivyokuwa katika ile Hema; vitu hivyo makuhani na Walawi wakavipandisha.

Na wana wa Walawi wakalichukua sanduku la Mungu mabegani mwao kwa miti yake, kama vile Musa alivyoamuru, kulingana na neno la BWANA.

Basi Daudi, na wazee wa Israeli, na makamanda wa maelfu, wakaenda, ili kulipandisha sanduku la Agano la BWANA kutoka nyumbani mwa Obed-edomu kwa furaha kuu;

Agano alilofanya na Abrahamu, Na kiapo chake kwa Isaka;

Naye Obed-edomu alikuwa na wana; Shemaya mzaliwa wa kwanza, Yehozabadi wa pili, Yoa wa tatu, na Sakari wa nne, na Nethaneli wa tano;

Amieli wa sita, Isakari wa saba, Peulethai wa nane; kwa jinsi Mungu alivyombariki.

Ndipo Sulemani alipowakusanya wazee wa Israeli, na wakuu wote wa kabila, wakuu wa mbari za mababa wa wana wa Israeli, huko Yerusalemu, ili walipandishe sanduku la Agano la BWANA kutoka mji wa Daudi, yaani, Sayuni.

Na mtu awaye yote atakayemnywesha mmojawapo wa wadogo hawa angaa kikombe cha maji baridi, kwa kuwa ni mwanafunzi, amin, nawaambia, haitampotea kamwe thawabu yake.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo