Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

2 Samueli 19:35 - Swahili Revised Union Version

35 Sasa nina miaka themanini; nami je! Naweza kupambanua mema na mabaya? Mimi mtumishi wako, je! Naweza kuonja nilacho au ninywacho? Naweza kusikia tena sauti ya waimbaji wa kiume na wa kike? Kwa nini basi mtumishi wako azidi kumlemea bwana wangu mfalme?

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

35 Mimi leo nina umri wa miaka themanini. Je, nina uwezo wa kubainisha yaliyo mazuri na yale yasiyo mazuri? Je, mimi mtumishi wako, naweza kutambua ladha ya kile ninachokula au kunywa? Je, nitaweza kutambua uzuri wa sauti za waimbaji wanaume au wanawake? Kwa nini mimi mtumishi wako niwe mzigo wa ziada kwako, bwana wangu mfalme?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

35 Mimi leo nina umri wa miaka themanini. Je, nina uwezo wa kubainisha yaliyo mazuri na yale yasiyo mazuri? Je, mimi mtumishi wako, naweza kutambua ladha ya kile ninachokula au kunywa? Je, nitaweza kutambua uzuri wa sauti za waimbaji wanaume au wanawake? Kwa nini mimi mtumishi wako niwe mzigo wa ziada kwako, bwana wangu mfalme?

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

35 Sasa nina miaka themanini. Je, naweza kutofautisha kati ya lililo jema na lililo baya? Je, mtumishi wako anaweza kujua ladha ya kile anachokula au anachokunywa? Je, bado naweza kusikiliza sauti za waimbaji wa kiume na za wanawake? Kwa nini mtumishi wako aongeze mzigo kwa bwana wangu mfalme?

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

BIBLIA KISWAHILI

35 Sasa nina miaka themanini; nami je! Naweza kupambanua mema na mabaya? Mimi mtumishi wako, je! Naweza kuonja nilacho au ninywacho? Naweza kusikia tena sauti ya waimbaji wa kiume na wa kike? Kwa nini basi mtumishi wako azidi kumlemea bwana wangu mfalme?

Tazama sura Nakili

2 Samueli 19:35
15 Marejeleo ya Msalaba  

Mfalme akamwambia Absalomu, Sivyo, mwanangu, tusiende sote, tusije tukakulemea. Akamsihi sana; asikubali kwenda, ila akambariki.

Daudi akamwambia, Ukienda mbele pamoja nami, utakuwa mzigo kwangu;

Mtumishi wako ataka kuvuka Yordani tu pamoja na mfalme; tena mbona mfalme anilipie thawabu ya namna hii?

tena, zaidi ya hao, kulikuwa na watumishi wao wa kiume na wa kike, ambao walikuwa elfu saba, na mia tatu na thelathini na saba; nao walikuwa na waimbaji wa kiume na wa kike mia mbili.

tena zaidi ya hao, kulikuwa na watumishi wao wanaume kwa wanawake, ambao walikuwa elfu saba na mia tatu na thelathini na saba; kisha walikuwa na waimbaji wanaume kwa wanawake mia mbili arubaini na watano.

Je! Sikio silo lijaribulo maneno, Kama vile kaakaa lionjavyo chakula?

Je! Mna udhalimu ulimini mwangu? Je! Makaakaa yangu hayatambui mambo ya madhara?

Miaka ya maisha yetu ni sabini, Na ikiwa tuna nguvu miaka themanini; Tena kiburi chake ni taabu na ubatili, Maana wakati unapita upesi nasi kutokomea punde.

na ikiwa watu wa nyumba ni wachache kwa mwana-kondoo, basi yeye na jirani yake aliye karibu na nyumba yake na watwae mwana-kondoo mmoja, kwa kadiri ya hesabu ya watu; kwa kadiri ya ulaji wa kila mtu, ndivyo mtakavyofanya hesabu yenu kwa yule mwana-kondoo.

Binti Farao akamwambia, Haya! Nenda. Yule kijana akaenda akamwita mama yake yule mtoto.

tena nikajikusanyia fedha na dhahabu, na tunu za kifalme na za kutoka katika majimbo. Nikajipatia waimbaji, wanaume kwa wanawake, nao wale ambao wanadamu wanawatunuka, masuria wengi sana.

Lakini chakula kigumu ni cha watu wazima, ambao akili zao, kwa kutumiwa, zimezoeshwa kupambanua mema na mabaya.

ikiwa mmeonja ya kwamba Bwana ni mwenye fadhili.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo