Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




2 Samueli 12:14 - Swahili Revised Union Version

14 Lakini, kwa kuwa kwa tendo hili umewapa adui za BWANA nafasi kubwa ya kukufuru, mtoto atakayezaliwa kwako hakika atakufa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 Hata hivyo, kwa kuwa kwa tendo lako umemdharau kabisa Mwenyezi-Mungu, mtoto wako atakufa.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

14 Hata hivyo, kwa kuwa kwa tendo lako umemdharau kabisa Mwenyezi-Mungu, mtoto wako atakufa.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 Hata hivyo, kwa kuwa kwa tendo lako umemdharau kabisa Mwenyezi-Mungu, mtoto wako atakufa.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 Lakini kwa sababu kwa kufanya hili umefanya adui za Mwenyezi Mungu kuonesha dharau kabisa, mwana atakayezaliwa kwako atakufa.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 Lakini kwa sababu kwa kufanya hili umefanya adui za bwana kuonyesha dharau kabisa, mwana atakayezaliwa kwako atakufa.”

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

14 Lakini, kwa kuwa kwa tendo hili umewapa adui za BWANA nafasi kubwa ya kukufuru, mtoto atakayezaliwa kwako hakika atakufa.

Tazama sura Nakili




2 Samueli 12:14
16 Marejeleo ya Msalaba  

Naye Nathani akaondoka kwenda nyumbani kwake. Basi BWANA akampiga yule mtoto ambaye mkewe Uria alimzalia Daudi naye akawa mgonjwa sana.


Tena nilisema, Neno hili mnalolitenda si jema; je! Haiwapasi ninyi kwenda katika kicho cha Mungu wetu, kwa sababu ya mashutumu ya makafiri adui zetu?


Wanaokungoja Wewe wasiaibishwe, Kwa ajili yangu, Bwana, MUNGU wa majeshi. Wanaokutafuta Wewe wasifedheheshwe, Kwa ajili yangu, Ee Mungu wa Israeli.


Ee Mungu, mtesi atalaumu hata lini? Adui alidharau jina lako hata milele?


Ee BWANA, heri mtu yule umwadibuye, Na kumfundisha kwa sheria yako;


Ee BWANA, Mungu wetu, ndiwe uliyewajibu; Ulikuwa kwao Mungu mwenye kusamehe Ingawa uliwapatiliza matendo yao.


Basi sasa, nafanya nini hapa, asema BWANA, ikiwa watu wangu wamechukuliwa bure? Hao wanaowatawala wanapiga yowe, asema BWANA, na jina langu linatukanwa daima mchana kutwa.


Ni ninyi tu niliowajua katika jamaa zote zilizo duniani; kwa sababu hiyo nitawapatiliza ninyi maovu yenu yote.


Ole ni wa ulimwengu kwa sababu ya mambo ya kukosesha! Maana hayana budi kuja mambo ya kukosesha; lakini ole wake mtu yule aliletaye jambo la kukosesha!


Kwa maana jina la Mungu latukanwa katika Mataifa kwa ajili yenu, kama ilivyoandikwa.


Ila tuhukumiwapo, twarudiwa na Bwana, isije ikatupasa adhabu pamoja na dunia.


Maana yeye ambaye Bwana ampenda, humuonya Naye humpiga kila mwana amkubaliye.


Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo