Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

1 Wafalme 7:2 - Swahili Revised Union Version

2 Kisha alijenga nyumba ya msitu wa Lebanoni; mikono mia moja urefu wake, na mikono hamsini upana wake, na mikono thelathini kwenda juu kwake, juu ya safu nne za nguzo za mwerezi, na mihimili ya mwerezi juu ya nguzo.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 Kisha, akajenga jengo lililoitwa Nyumba ya Msitu wa Lebanoni. Urefu wake ulikuwa mita 44.5, upana wake mita 22.25, na kimo chake mita 13.5. Ilikuwa imejengwa juu ya safu 3 za nguzo za mierezi, nguzo ambazo zilishikilia boriti za mierezi kwa upande wa juu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 Kisha, akajenga jengo lililoitwa Nyumba ya Msitu wa Lebanoni. Urefu wake ulikuwa mita 44.5, upana wake mita 22.25, na kimo chake mita 13.5. Ilikuwa imejengwa juu ya safu 3 za nguzo za mierezi, nguzo ambazo zilishikilia boriti za mierezi kwa upande wa juu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 Alijenga jumba lililoitwa Jumba la Kifalme la Msitu wa Lebanoni. Lilikuwa na urefu wa dhiraa mia moja, upana wa dhiraa hamsini, na kimo cha dhiraa thelathini, na safu nne za nguzo za mwerezi zilizoshikilia boriti za mwerezi zilizosawazishwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 Alijenga Jumba la Kifalme la Msitu wa Lebanoni, urefu wake ulikuwa dhiraa 100, upana wake dhiraa hamsini na kimo chake dhiraa thelathini, likiwa na safu nne za nguzo za mierezi zikishikilia boriti za mierezi zilizorembwa.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

2 Kisha alijenga nyumba ya msitu wa Lebanoni; mikono mia moja urefu wake, na mikono hamsini upana wake, na mikono thelathini kwenda juu kwake, juu ya safu nne za nguzo za mwerezi, na mihimili ya mwerezi juu ya nguzo.

Tazama sura Nakili

1 Wafalme 7:2
8 Marejeleo ya Msalaba  

Na vigao mia tatu vya dhahabu iliyofuliwa; kila kigao kimoja kilipata mane tatu za dhahabu. Mfalme akaviweka katika nyumba ya msitu wa Lebanoni.

Na vyombo vyote vya kunywea vya mfalme Sulemani vilikuwa vya dhahabu, na vyombo vyote vya nyumba ya msitu wa Lebanoni vilikuwa vya dhahabu iliyosafika; hakuna vya fedha, fedha haikuhesabiwa kuwa kitu siku za Sulemani.

Ikafunikwa juu kwa mwerezi juu ya mihimili arubaini na mitano, iliyokuwa juu ya nguzo; kumi na mitano kwa safu.

Ikawa Sulemani alipokwisha kuijenga nyumba ya BWANA, na nyumba ya mfalme, na mambo yote yaliyoingia moyoni mwake Sulemani, naye akataka kuyafanya,

na miji yote ya hazina iliyokuwa yake Sulemani; na miji ya magari yake, na miji ya watu wake wapandao farasi, na kila alichopenda kujenga Sulemani huko Yerusalemu, na katika Lebanoni, na katika nchi yote ya mamlaka yake.

Na vigao mia tatu vya dhahabu iliyofuliwa; kigao kimoja hupata shekeli mia tatu za dhahabu; mfalme akaviweka katika nyumba ya msitu wa Lebanoni.

Shingo yako ni kama huo mnara wa pembe; Macho yako kama viziwa vya Heshboni, Karibu na mlango wa Beth-rabi; Pua yako ni kama mnara wa Lebanoni, Unaoelekea Dameski;

Kisha alikiondoa kifuniko cha Yuda, nawe siku hiyo ulivitazama vyombo vya vita katika nyumba ya mwituni.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo