Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




1 Samueli 2:1 - Swahili Revised Union Version

1 Naye Hana akaomba, akasema, Moyo wangu wamshangilia BWANA, Pembe yangu imetukuka katika BWANA, Kinywa changu kimepanuka juu ya adui zangu; Kwa kuwa naufurahia wokovu wako;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Halafu Hana aliomba na kusema: “Namshangilia Mwenyezi-Mungu moyoni mwangu. Namtukuza Mwenyezi-Mungu aliye nguvu yangu. Nawacheka adui zangu; maana naufurahia ushindi wangu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Halafu Hana aliomba na kusema: “Namshangilia Mwenyezi-Mungu moyoni mwangu. Namtukuza Mwenyezi-Mungu aliye nguvu yangu. Nawacheka adui zangu; maana naufurahia ushindi wangu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Halafu Hana aliomba na kusema: “Namshangilia Mwenyezi-Mungu moyoni mwangu. Namtukuza Mwenyezi-Mungu aliye nguvu yangu. Nawacheka adui zangu; maana naufurahia ushindi wangu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Kisha Hana akaomba na kusema: “Moyo wangu wamshangilia Mwenyezi Mungu, katika Mwenyezi Mungu pembe yangu imeinuliwa juu. Kinywa changu chajisifu juu ya adui zangu, kwa kuwa naufurahia wokovu wako.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Kisha Hana akaomba na kusema: “Moyo wangu wamshangilia bwana, katika bwana pembe yangu imeinuliwa juu. Kinywa changu chajisifu juu ya adui zangu, kwa kuwa naufurahia wokovu wako.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

1 Naye Hana akaomba, akasema, Moyo wangu wamshangilia BWANA, Pembe yangu imetukuka katika BWANA, Kinywa changu kimepanuka juu ya adui zangu; Kwa kuwa naufurahia wokovu wako;

Tazama sura Nakili




1 Samueli 2:1
37 Marejeleo ya Msalaba  

Kisha wakarudi, kila mtu wa Yuda na Yerusalemu, na Yehoshafati mbele yao, ili kuurudia Yerusalemu kwa furaha; kwa kuwa BWANA amewafurahisha juu ya adui zao.


na Matania, mwana wa Mika, mwana wa Zikri, mwana wa Asafu, mkuu wa kuanzisha shukrani katika sala, na Bakbukia, wa pili wake miongoni mwa nduguze; na Obadia, mwana wa Shemaya, mwana wa Galali, mwana wa Yeduthuni.


Nimeshona nguo ya magunia juu ya mwili wangu, Na nguvu zangu nimezibwaga mavumbini.


BWANA ni nguvu zangu na wimbo wangu, Naye amekuwa wokovu wangu.


Lakini mimi nimezitumainia fadhili zako; Moyo wangu na uufurahie wokovu wako.


Naye amewainulia watu wake pembe, Sifa za watauwa wake wote; Wana wa Israeli, watu walio karibu naye. Haleluya.


BWANA ni jabali langu, na boma langu, na mwokozi wangu, Mungu wangu, mwamba wangu ninayemkimbilia, Ngao yangu, na pembe ya wokovu wangu, na ngome yangu.


Na tuushangilie wokovu wako, Kwa jina la Mungu wetu tuzitweke bendera zetu. BWANA akutimizie matakwa yako yote.


Umempa haja ya moyo wake, Wala hukumzuilia matakwa ya midomo yake.


Na nafsi yangu itamfurahia BWANA, Na kuushangilia wokovu wake.


Ee Bwana, uifumbue midomo yangu, Na kinywa changu kitazinena sifa zako.


Kinywa changu kitajazwa sifa zako, Na heshima yako mchana kutwa.


Nguvu zote za wasio haki nitazimaliza, Lakini nguvu za mwenye haki nitaziimarisha.


Maana fahari ya nguvu zao ni Wewe, Na kwa radhi yako pembe yetu itatukuka.


Maana ngao yetu ni BWANA, Na mfalme wetu ni wake Mtakatifu wa Israeli.


Uaminifu wangu na fadhili zangu atakuwa nazo, Na kwa jina langu pembe yake itatukuka.


Ili nizisimulie sifa zako zote; Katika malango ya binti Sayuni Nitaufurahia wokovu wako.


Bali pembe yangu umeiinua kama pembe ya nyati, Nimepakwa mafuta mabichi.


Ndipo Musa na wana wa Israeli wakamwimbia BWANA wimbo huu wakanena, na kusema, Nitamwimbia BWANA, kwa maana ametukuka sana; Farasi na mpanda farasi amewatupa baharini.


Miriamu akawaitikia, Mwimbieni BWANA kwa maana ametukuka sana; Farasi na mpanda farasi amewatupa baharini.


Sala ya nabii Habakuki.


Walakini nitamfurahia BWANA Nitamshangilia Mungu wa wokovu wangu.


Ametusimamishia pembe ya wokovu Katika mlango wa Daudi, mtumishi wake.


Wala si hivyo tu, ila pia twajifurahisha katika Mungu kwa Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa yeye sasa tumeupokea huo upatanisho.


Mzaliwa wa kwanza wa ng'ombe wake mume, enzi ni yake; Na pembe zake ni pembe za nyati; Kwa hizo atayasukuma mataifa yote, hata ncha za nchi; Nao ni makumi ya maelfu ya Efraimu, Nao ni maelfu ya Manase.


Maana sisi tu tohara, tumwabuduo Mungu kwa Roho, na kuona fahari juu ya Kristo Yesu, wala hatuutumainii mwili.


Furahini katika Bwana sikuzote; tena nasema, Furahini.


Msijisumbue kwa neno lolote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu.


Naye mwampenda, ijapokuwa hamkumwona; ambaye ijapokuwa hamumwoni sasa, mnamwamini; na kufurahi sana, kwa furaha isiyoneneka, yenye utukufu,


Furahini juu yake, enyi mbingu, na enyi watakatifu, mitume na manabii; kwa maana Mungu ametoa hukumu kwa ajili yenu juu yake.


Ila mwenzake humchokoza sana, ili kumwuudhi, kwa sababu BWANA alikuwa amemfunga tumbo.


Tena mumewe akafanya hivyo mwaka kwa mwaka, hapo yule mwanamke alipokwea kwenda nyumbani kwa BWANA, ndivyo yule alivyomchokoza; basi, kwa hiyo, yeye akalia, asile chakula.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo