Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

1 Samueli 14:52 - Swahili Revised Union Version

52 Tena, kulikuwa na vita kali sana juu ya Wafilisti siku zote za Sauli, naye Sauli alipomwona mtu yeyote aliyekuwa hodari, au mtu yeyote aliyekuwa shujaa, humtwaa ili awe pamoja naye.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

52 Kulikuwa na mapigano makali dhidi ya Wafilisti muda wote Shauli alipokuwa mfalme; na kila mara Shauli alipompata mtu mwenye nguvu au shujaa alimchukua ajiunge na jeshi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

52 Kulikuwa na mapigano makali dhidi ya Wafilisti muda wote Shauli alipokuwa mfalme; na kila mara Shauli alipompata mtu mwenye nguvu au shujaa alimchukua ajiunge na jeshi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

52 Kulikuwa na mapigano makali dhidi ya Wafilisti muda wote Shauli alipokuwa mfalme; na kila mara Shauli alipompata mtu mwenye nguvu au shujaa alimchukua ajiunge na jeshi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

52 Siku zote za utawala wa Sauli zilikuwa za vita vikali dhidi ya Wafilisti, na wakati wowote Sauli alimwona mtu mwenye nguvu au shujaa, alimchukua kwa utumishi wake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

52 Siku zote za utawala wa Sauli zilikuwa za vita vikali dhidi ya Wafilisti, na wakati wowote Sauli alimwona mtu mwenye nguvu au shujaa, alimchukua kwa utumishi wake.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

52 Tena, kulikuwa na vita kali sana juu ya Wafilisti siku zote za Sauli, naye Sauli alipomwona mtu yeyote aliyekuwa hodari, au mtu yeyote aliyekuwa shujaa, humtwaa ili awe pamoja naye.

Tazama sura Nakili

1 Samueli 14:52
4 Marejeleo ya Msalaba  

Nao Wafilisti wakakusanyika ili wapigane na Waisraeli, magari elfu thelathini, na wapanda farasi elfu sita, na watu kama mchanga ulio ufuoni mwa bahari kwa wingi wao; wakapanda juu, wakapiga kambi yao katika Mikmashi, upande wa mashariki wa Beth-aveni.

Basi Sauli alipokwisha kuutwaa ufalme juu ya Israeli, alipigana na adui zake wote pande zote, juu ya Moabu, na juu ya wana wa Amoni, na juu ya Edomu, na juu ya wafalme wa Soba, na juu ya Wafilisti; na popote alipogeukia, akawashinda.

Na Samweli alipozeeka, aliwafanya wanawe wawe waamuzi juu ya Israeli.

Akasema, Mfalme atakayewatawala ninyi atakuwa na desturi hii; atatwaa wana wenu na kuwaweka kwake, katika magari yake, na kuwa wapanda farasi wake; nao watapiga mbio mbele ya magari yake.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo