Akajipanga apigane nao usiku, yeye na watumwa wake, akawapiga, akawafukuza mpaka Hoba, ulioko upande wa kushoto wa Dameski.
Zekaria 9:1 - Swahili Revised Union Version Ufunuo wa neno la BWANA, lililosemwa juu ya nchi ya Hadraki, na Dameski itakuwa mahali pake pa kustarehe; kwa maana jicho la mwanadamu na la kabila zote za Israeli linamwelekea BWANA; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kauli ya Mwenyezi-Mungu: Mwenyezi-Mungu ametamka siyo tu dhidi ya nchi ya Hadraki bali pia dhidi ya Damasko. Maana nchi ya Aramu ni mali ya Mwenyezi-Mungu, kama vile yalivyo makabila yote ya Israeli. Biblia Habari Njema - BHND Kauli ya Mwenyezi-Mungu: Mwenyezi-Mungu ametamka siyo tu dhidi ya nchi ya Hadraki bali pia dhidi ya Damasko. Maana nchi ya Aramu ni mali ya Mwenyezi-Mungu, kama vile yalivyo makabila yote ya Israeli. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kauli ya Mwenyezi-Mungu: Mwenyezi-Mungu ametamka siyo tu dhidi ya nchi ya Hadraki bali pia dhidi ya Damasko. Maana nchi ya Aramu ni mali ya Mwenyezi-Mungu, kama vile yalivyo makabila yote ya Israeli. Neno: Bibilia Takatifu Neno la unabii: Neno la Mwenyezi Mungu liko kinyume na nchi ya Hadraki na Dameski itakuwa mahali pa kupumzika, kwa kuwa macho ya watu na ya makabila yote ya Israeli yako kwa Mwenyezi Mungu; Neno: Maandiko Matakatifu Neno: Neno la bwana liko kinyume na nchi ya Hadraki na Dameski itakuwa mahali pa kupumzika, kwa kuwa macho ya watu na ya kabila zote za Israeli yako kwa bwana, BIBLIA KISWAHILI Ufunuo wa neno la BWANA, lililosemwa juu ya nchi ya Hadraki, na Dameski itakuwa mahali pake pa kustarehe; kwa maana jicho la mwanadamu na la kabila zote za Israeli linamwelekea BWANA; |
Akajipanga apigane nao usiku, yeye na watumwa wake, akawapiga, akawafukuza mpaka Hoba, ulioko upande wa kushoto wa Dameski.
Ee Mungu wetu, je! Hutawahukumu? Maana sisi hatuna uwezo juu ya jamii kubwa hii, wanaotujia juu yetu; wala hatujui tufanyeje; lakini macho yetu yanatazama kwako.
BWANA ameweka wazi mkono wake mtakatifu Machoni pa mataifa yote; Na ncha zote za dunia Zitauona wokovu wa Mungu wetu.
Ee BWANA, nguvu zangu, ngome yangu, na kimbilio langu siku ya taabu, kwako wewe watakuja mataifa yote toka ncha za dunia, wakisema, Baba zenu hawakurithi kitu ila uongo, naam, ubatili na vitu visivyofaa.
mkuu wa mashauri, muweza katika kutenda; ambaye macho yake yamefumbuka juu ya njia zote za wanadamu, kumpa kila mtu kwa kadiri ya njia zake, na kwa kadiri ya matunda ya matendo yake,
Haya ndiyo asemayo BWANA; Kwa makosa matatu ya Tiro, naam, kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate; kwa sababu wameitia kabila nzima katika mikono ya Edomu, wala hawakulikumbuka agano la udugu;
Haya ndiyo asemayo BWANA; Kama vile mchungaji apokonyavyo kinywani mwa simba miguu miwili, au kipande cha sikio; ndivyo watakavyopokonywa wana wa Israeli, wakaao Samaria katika pembe ya kochi, na juu ya mito ya hariri ya kitanda.
Maana yeyote aliyeidharau siku ya mambo madogo watafurahi, naye ataiona timazi ikiwa katika mkono wa Zerubabeli; naam, hizi taa saba ndizo macho ya BWANA; yanaona huku na huko duniani kote.
Nitaituma itokee, asema BWANA wa majeshi, nayo itaingia katika nyumba ya mwizi, na katika nyumba ya yeyote aapaye kwa uongo kwa jina langu; nayo itakaa katika nyumba yake, na kuiteketeza, pamoja na boriti zake na mawe yake.