Kwa sababu nilimwokoa maskini aliyenililia; Yatima naye, na yule asiyekuwa na mtu wa kumsaidia.
Zaburi 82:3 - Swahili Revised Union Version Mfanyieni hukumu maskini na yatima; Mtendeeni haki aliyeonewa, na fukara; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wapeni wanyonge na yatima haki zao; tekelezeni haki za wanaoonewa na fukara. Biblia Habari Njema - BHND Wapeni wanyonge na yatima haki zao; tekelezeni haki za wanaoonewa na fukara. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wapeni wanyonge na yatima haki zao; tekelezeni haki za wanaoonewa na fukara. Neno: Bibilia Takatifu Teteeni wanyonge na yatima, tunzeni haki za maskini na waliodhulumiwa. Neno: Maandiko Matakatifu Teteeni wanyonge na yatima, tunzeni haki za maskini na walioonewa. BIBLIA KISWAHILI Mfanyieni hukumu maskini na yatima; Mtendeeni haki aliyeonewa, na fukara; |
Kwa sababu nilimwokoa maskini aliyenililia; Yatima naye, na yule asiyekuwa na mtu wa kumsaidia.
jifunzeni kutenda mema; takeni hukumu na haki; wasaidieni walioonewa; mpatieni yatima haki yake; mteteeni mjane.
Wakuu wako ni waasi, na rafiki za wezi; kila mtu hupenda rushwa, hufuata malipo; hawampatii yatima haki yake, wala maneno ya mjane hayawafikii.
Ee nyumba ya Daudi, BWANA asema hivi, Hukumuni hukumu ya haki asubuhi, mkawaponye waliotekwa nyara na mkono wake aliyewadhulumu, ghadhabu yangu isije ikatoka kama moto, ikaunguza, asiweze mtu yeyote kuuzima, kwa sababu ya uovu wa matendo yenu.
Alihukumu maneno ya maskini na mhitaji; hapo ndipo alipofanikiwa. Je! Huku siko kunijua, asema BWANA?
BWANA asema hivi, Fanyeni hukumu na haki, mkamtoe yeye aliyetekwa katika mikono ya mdhalimu; wala msiwatende mabaya mgeni, wala yatima, wala mjane, wala kuwadhulumu, wala msimwage damu ya mtu asiye na hatia katika mahali hapa.
Wamenenepa sana, wang'aa; naam, wamepita kiasi kwa matendo maovu; hawatetei madai ya yatima, ili wapate kufanikiwa; wala hawaamui haki ya mhitaji.
BWANA wa majeshi amesema hivi, ya kwamba, Fanyeni hukumu za kweli, kila mtu na amwonee ndugu yake rehema na huruma;
Huwafanyia yatima na mjane hukumu ya haki, naye humpenda mgeni, akimpa chakula na mavazi.
Dini iliyo safi, isiyo na dosari mbele za Mungu Baba ni hii, Kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo mawaa.