Zaburi 102:16 - Swahili Revised Union Version BWANA atakapokuwa ameijenga Sayuni, Atakapoonekana katika utukufu wake, Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwenyezi-Mungu ataijenga upya Siyoni, na kuonekana alivyo mtukufu. Biblia Habari Njema - BHND Mwenyezi-Mungu ataijenga upya Siyoni, na kuonekana alivyo mtukufu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwenyezi-Mungu ataijenga upya Siyoni, na kuonekana alivyo mtukufu. Neno: Bibilia Takatifu Kwa maana Mwenyezi Mungu ataijenga tena Sayuni na kutokea katika utukufu wake. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa maana bwana ataijenga tena Sayuni na kutokea katika utukufu wake. BIBLIA KISWAHILI BWANA atakapokuwa ameijenga Sayuni, Atakapoonekana katika utukufu wake, |
Maana Mungu ataiokoa Sayuni, na kuijenga miji ya Yuda, Na watu watakaa ndani yake na kuimiliki.
Hilo ndilo kusudi lililokusudiwa duniani kote, na huo ndio mkono ulionyoshwa juu ya mataifa yote.
Basi, wataliogopa jina la BWANA toka magharibi, na utukufu wake toka maawio ya jua; maana yeye atakuja kama mkondo wa mto ufurikao, uendeshwao kwa pumzi ya BWANA.
Makundi yote ya Kedari yatakusanyika kwako, Kondoo dume wa Nebayothi watakutumikia; Watapanda juu ya madhabahu yangu kwa kibali, Nami nitaitukuza nyumba ya utukufu wangu.
kuwaagizia hao waliao katika Sayuni, wapewe taji la maua badala ya majivu, mafuta ya furaha badala ya maombolezo, vazi la sifa badala ya roho nzito; wapate kuitwa miti ya haki, iliyopandwa na BWANA, ili atukuzwe.
Nami nayajua matendo yao na mawazo yao; wakati unakuja nitakapokusanya mataifa yote na lugha zote; nao watakuja, nao watauona utukufu wangu.
Mara ya pili nitakujenga, nawe utajengwa, Ee bikira wa Israeli mara ya pili utapambwa kwa matari yako, nawe utatokea katika michezo yao wanaofurahi.
Wanawake wa watu wangu mnawatupa nje ya nyumba zao nzuri; watoto wao wachanga mnawanyang'anya utukufu wangu milele.
Lakini na alaaniwe mtu adanganyaye, ambaye katika kundi lake ana dume, akaweka nadhiri, ila amtolea Bwana kitu kilicho na kilema; kwa maana mimi ni Mfalme mkuu, asema BWANA wa majeshi, na jina langu latisha katika mataifa.