Kisha Yoshua aliambiwa habari hiyo, ya kwamba, Hao wafalme watano wameonekana, nao wamejificha ndani ya pango ya Makeda
Yoshua 8:23 - Swahili Revised Union Version Kisha wakamshika mfalme wa Ai akiwa hai, nao wakamleta kwa Yoshua. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini mfalme wa mji wa Ai walimteka akiwa hai na kumpeleka kwa Yoshua. Biblia Habari Njema - BHND Lakini mfalme wa mji wa Ai walimteka akiwa hai na kumpeleka kwa Yoshua. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini mfalme wa mji wa Ai walimteka akiwa hai na kumpeleka kwa Yoshua. Neno: Bibilia Takatifu Lakini wakamchukua mfalme wa Ai akiwa hai na kumleta kwa Yoshua. Neno: Maandiko Matakatifu Lakini wakamchukua mfalme wa Ai akiwa hai na kumleta kwa Yoshua. BIBLIA KISWAHILI Kisha wakamshika mfalme wa Ai akiwa hai, nao wakamleta kwa Yoshua. |
Kisha Yoshua aliambiwa habari hiyo, ya kwamba, Hao wafalme watano wameonekana, nao wamejificha ndani ya pango ya Makeda
Kisha Yoshua akasema, Haya, funua mdomo wa pango, mniletee hao wafalme watano hapa nje ya pango.
Tena hao; wengine wakatoka nje ya mji huo kinyume chao; hivyo basi wakawa katikati ya Waisraeli, wengine upande huu na wengine upande ule; nao wakawapiga, hata wasimwache hata mmoja miongoni mwao aliyesalia, wala kupona.
Kisha ikawa, hapo Israeli walipokuwa wamekwisha kuwaua wenyeji wote wa Ai katika bara, hapo katika nyika walipokuwamo wakiwafuatia, nao walikuwa wamekwisha anguka wote kwa makali ya upanga, hadi walipokuwa wameangamizwa wote, ndipo Israeli wakarejea Ai, na kuupiga huo mji kwa makali ya upanga.
Na huyo mfalme wa Ai akamtundika katika mti hadi wakati wa jioni; kisha hapo jua lilipokuchwa Yoshua akaagiza, nao wakauondoa mzoga wake katika huo mti, na kuutupa hapo penye maingilio ya lango la mji, kisha wakaweka pale juu yake rundo kubwa la mawe, hata hivi leo.
Yule mnyama akakamatwa, na yule nabii wa uongo pamoja naye, yeye aliyezifanya hizo ishara mbele yake, ambazo kwa hizo aliwadanganya watu wale walioipokea ile chapa ya huyo mnyama, nao hao walioisujudia sanamu yake; hao wawili wakatupwa wakiwa hai katika lile ziwa la moto liwakalo kwa kiberiti;
Akamkamata Agagi, mfalme wa Waamaleki akiwa hai, akawaangamiza hao watu wote kwa upanga.