Abrahamu akaondoka alfajiri, akatandika punda wake, akachukua vijana wawili pamoja naye, na Isaka mwanawe, akachanja kuni kwa ajili ya hiyo sadaka ya kuteketezwa, akaondoka, akaenda mpaka mahali alipoambiwa na Mungu.
Yoshua 8:10 - Swahili Revised Union Version Yoshua akaamka asubuhi na mapema, akawakutanisha watu, kisha akatangulia kukwea kwenda Ai mbele ya hao watu, yeye na wazee wa Israeli. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Yoshua akaamka asubuhi na mapema, akawakusanya Waisraeli na kuelekea mjini Ai, akiwa pamoja na wazee. Biblia Habari Njema - BHND Yoshua akaamka asubuhi na mapema, akawakusanya Waisraeli na kuelekea mjini Ai, akiwa pamoja na wazee. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Yoshua akaamka asubuhi na mapema, akawakusanya Waisraeli na kuelekea mjini Ai, akiwa pamoja na wazee. Neno: Bibilia Takatifu Asubuhi na mapema siku iliyofuata, Yoshua akakusanya jeshi lake, na yeye na viongozi wa Israeli wakawaongoza kwenda Ai. Neno: Maandiko Matakatifu Asubuhi na mapema siku iliyofuatia, Yoshua akawakutanisha watu wake, na yeye na viongozi wa Israeli wakawa mbele ya watu kwenda Ai. BIBLIA KISWAHILI Yoshua akaamka asubuhi na mapema, akawakutanisha watu, kisha akatangulia kukwea kwenda Ai mbele ya hao watu, yeye na wazee wa Israeli. |
Abrahamu akaondoka alfajiri, akatandika punda wake, akachukua vijana wawili pamoja naye, na Isaka mwanawe, akachanja kuni kwa ajili ya hiyo sadaka ya kuteketezwa, akaondoka, akaenda mpaka mahali alipoambiwa na Mungu.
Yoshua akaondoka asubuhi na mapema, nao wakatoka Shitimu, wakafika katika mto wa Yordani, yeye na wana wa Israeli wote, wakakaa hapo kabla ya kuvuka.
Basi Yoshua akaondoka asubuhi na mapema, akawasongeza Israeli kabila kwa kabila; kabila la Yuda likatwaliwa.
Watu wote, hao wa vita, waliokuwa pamoja naye, wakaenda wakakaribia, na kufika mbele ya mji, wakatua upande wa kaskazini wa Ai; napo palikuwa na bonde kati yao na Ai.
Basi Yoshua akawatuma; nao wakaenda hadi hapo watakapootea, wakakaa kati ya Betheli na Ai, upande wa magharibi wa Ai; lakini Yoshua akalala usiku huo kati ya watu.