Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Mwanzo 22:3 - Swahili Revised Union Version

3 Abrahamu akaondoka alfajiri, akatandika punda wake, akachukua vijana wawili pamoja naye, na Isaka mwanawe, akachanja kuni kwa ajili ya hiyo sadaka ya kuteketezwa, akaondoka, akaenda mpaka mahali alipoambiwa na Mungu.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 Basi, kesho yake, Abrahamu akaamka asubuhi na mapema, akatandika punda wake, akawachukua watumishi wake wawili pamoja na Isaka mwanawe. Akatayarisha kuni kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, kisha akaanza safari kuelekea mahali alipoambiwa na Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 Basi, kesho yake, Abrahamu akaamka asubuhi na mapema, akatandika punda wake, akawachukua watumishi wake wawili pamoja na Isaka mwanawe. Akatayarisha kuni kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, kisha akaanza safari kuelekea mahali alipoambiwa na Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 Ibrahimu akaamka asubuhi na mapema siku iliyofuata, akamtayarisha punda wake. Akawachukua watumishi wake wawili pamoja na Isaka mwanawe. Baada ya kuchanja kuni za kutosha kwa ajili ya hiyo sadaka ya kuteketezwa, akaondoka kuelekea mahali Mungu alipokuwa amemwambia.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

BIBLIA KISWAHILI

3 Abrahamu akaondoka alfajiri, akatandika punda wake, akachukua vijana wawili pamoja naye, na Isaka mwanawe, akachanja kuni kwa ajili ya hiyo sadaka ya kuteketezwa, akaondoka, akaenda mpaka mahali alipoambiwa na Mungu.

Tazama sura Nakili

Mwanzo 22:3
16 Marejeleo ya Msalaba  

Abrahamu akamtwaa Ishmaeli mwanawe, na wote waliozaliwa nyumbani mwake, na wote walionunuliwa kwa fedha yake, wanaume wote wa watu wa nyumba ya Abrahamu, akawatahiri nyama ya magovi yao siku ile ile, kama Mungu alivyomwambia.

Abrahamu akaamka asubuhi na mapema akatwaa mkate na kiriba cha maji, akampa Hajiri akamtwika begani pake, na kijana, akamruhusu; naye akatoka, akapotea katika jangwa la Beer-sheba.

na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia; kwa sababu umetii sauti yangu.

Akasema, Umchukue mwanao, mwana wako wa pekee, umpendaye, Isaka, ukaende zako mpaka nchi ya Moria, ukamtoe sadaka ya kuteketezwa huko juu ya mlima mmojawapo nitakaokuambia.

Siku ya tatu Abrahamu akainua macho yake, akapaona mahali pakiwa bado ni mbali.

Nilifanya haraka wala sikukawia, Kuyatii maagizo yako.

Lolote mkono wako utakalolipata kulifanya, ulifanye kwa nguvu zako; kwa kuwa hakuna kazi, wala shauri, wala maarifa, wala hekima, huko kuzimu uendako wewe.

Apendaye baba au mama kuliko mimi, hanistahili; wala apendaye mwana au binti kuliko mimi, hanistahili.

Kama mtu akija kwangu naye hamchukii baba yake, na mama yake, na mke wake, na wanawe, na ndugu zake wa kiume na wa kike; naam, na hata nafsi yake mwenyewe, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.

alipoona vema kumdhihirisha Mwanawe ndani yangu, ili niwahubirie Mataifa habari zake; mara sikufanya shauri na watu wenye mwili na damu;

Kwa imani Abrahamu alipoitwa aliitika, atoke aende mahali pale atakapopapata kuwa urithi; akatoka asijue aendako.

Yoshua akaondoka asubuhi na mapema, nao wakatoka Shitimu, wakafika katika mto wa Yordani, yeye na wana wa Israeli wote, wakakaa hapo kabla ya kuvuka.

Yoshua akaamka asubuhi na mapema, akawakutanisha watu, kisha akatangulia kukwea kwenda Ai mbele ya hao watu, yeye na wazee wa Israeli.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo