Yoshua 7:14 - Swahili Revised Union Version Basi asubuhi mtaletwa karibu nami kabila kwa kabila; kisha itakuwa ya kwamba kabila ile atakayoitwaa BWANA itakaribia jamaa kwa jamaa; na jamaa ile atakayoitwaa BWANA itakaribia nyumba kwa nyumba; na nyumba ile atakayoitwaa BWANA itakaribia mtu kwa mtu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kwa hiyo kesho asubuhi wote mtakuja mbele yangu, kabila baada ya kabila. Kabila nitakalolichagua litakwenda mbele, ukoo baada ya ukoo. Ukoo nitakaouchagua utakwenda mbele, jamaa baada ya jamaa. Na jamaa nitakayoichagua itakwenda mbele, mtu mmojammoja. Biblia Habari Njema - BHND Kwa hiyo kesho asubuhi wote mtakuja mbele yangu, kabila baada ya kabila. Kabila nitakalolichagua litakwenda mbele, ukoo baada ya ukoo. Ukoo nitakaouchagua utakwenda mbele, jamaa baada ya jamaa. Na jamaa nitakayoichagua itakwenda mbele, mtu mmojammoja. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kwa hiyo kesho asubuhi wote mtakuja mbele yangu, kabila baada ya kabila. Kabila nitakalolichagua litakwenda mbele, ukoo baada ya ukoo. Ukoo nitakaouchagua utakwenda mbele, jamaa baada ya jamaa. Na jamaa nitakayoichagua itakwenda mbele, mtu mmojammoja. Neno: Bibilia Takatifu “ ‘Asubuhi, mtakuja kabila kwa kabila. Kisha kabila atakalolichagua Mwenyezi Mungu watakuja mbele kufuatana na koo zao; nao ukoo atakaouchagua Mwenyezi Mungu watakuja mbele jamaa kwa jamaa, nayo jamaa atakayoichagua Mwenyezi Mungu watakuja mbele mtu kwa mtu. Neno: Maandiko Matakatifu “ ‘Asubuhi, mjihudhurishe kabila kwa kabila. Itakuwa kabila lile atakalolitwaa bwana litakuja mbele ukoo kwa ukoo, ukoo ule atakaoutwaa bwana utakuja mbele jamaa kwa jamaa, nayo jamaa ile atakayoitwaa bwana itakuja mbele mtu kwa mtu. BIBLIA KISWAHILI Basi asubuhi mtaletwa karibu nami kabila kwa kabila; kisha itakuwa ya kwamba kabila ile atakayoitwaa BWANA itakaribia jamaa kwa jamaa; na jamaa ile atakayoitwaa BWANA itakaribia nyumba kwa nyumba; na nyumba ile atakayoitwaa BWANA itakaribia mtu kwa mtu. |
Wakasemezana kila mtu na mwenzake, Haya, na tupige kura, tupate kujua mabaya haya yametupata kwa sababu ya nani. Basi wakapiga kura, nayo kura ikamwangukia Yona.