Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Yoshua 7:15 - Swahili Revised Union Version

15 Tena itakuwa ya kwamba yeye atakayetwaliwa, naye anacho kitu kile kilichowekwa wakfu, atateketezwa kwa moto, yeye na vitu vyote alivyo navyo; kwa sababu amelivunja agano la BWANA, na kwa sababu ametenda upumbavu katika Israeli.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

15 Mtu yeyote atakayepatikana akiwa na vitu vilivyotolewa viangamizwe atateketezwa kwa moto, yeye pamoja na kila kitu chake maana ameliasi agano langu mimi Mwenyezi-Mungu, akatenda jambo la aibu katika Israeli.’”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

15 Mtu yeyote atakayepatikana akiwa na vitu vilivyotolewa viangamizwe atateketezwa kwa moto, yeye pamoja na kila kitu chake maana ameliasi agano langu mimi Mwenyezi-Mungu, akatenda jambo la aibu katika Israeli.’”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

15 Mtu yeyote atakayepatikana akiwa na vitu vilivyotolewa viangamizwe atateketezwa kwa moto, yeye pamoja na kila kitu chake maana ameliasi agano langu mimi Mwenyezi-Mungu, akatenda jambo la aibu katika Israeli.’”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

15 Yule atakayekutwa na vitu vilivyotengwa kwa ajili ya kuangamizwa, atateketezwa kwa moto pamoja na vitu vyote alivyo navyo. Kwa kuwa amelivunja agano la Mwenyezi Mungu na kufanya kitu cha aibu katika Israeli!’ ”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

15 Yule atakayekutwa na vitu vilivyowekwa wakfu, atateketezwa kwa moto, pamoja na vitu vyote alivyo navyo. Kwa kuwa amelivunja agano la bwana na kufanya kitu cha aibu katika Israeli!’ ”

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

15 Tena itakuwa ya kwamba yeye atakayetwaliwa, naye anacho kitu kile kilichowekwa wakfu, atateketezwa kwa moto, yeye na vitu vyote alivyo navyo; kwa sababu amelivunja agano la BWANA, na kwa sababu ametenda upumbavu katika Israeli.

Tazama sura Nakili

Yoshua 7:15
11 Marejeleo ya Msalaba  

Wanawe Yakobo waliposikia hayo, wakaja kutoka malishoni; nao wakasikitika sana, wakakasirika mno, kwa sababu amefanya upumbavu katika Israeli kwa kulala na binti Yakobo, jambo lisilostahili kutendeka.

Nami nichukue wapi aibu yangu? Wewe nawe utakuwa kama mmoja wa wapumbavu wa Israeli. Basi, sasa, nakusihi, useme na mfalme; kwa maana hatakukataza kunioa.

Israeli wamefanya dhambi, naam, wamelivunja agano langu nililowaagiza; naam, wametwaa baadhi ya vitu vilivyowekwa wakfu; tena wameiba, tena wameficha na kuvitia pamoja na vitu vyao wenyewe.

Basi Yoshua akaondoka asubuhi na mapema, akawasongeza Israeli kabila kwa kabila; kabila la Yuda likatwaliwa.

nasi tutatwaa watu kumi katika mia moja katika kabila zote za Israeli, na watu mia moja katika elfu, na watu elfu katika elfu kumi, ili waende kuwatwalia watu vyakula, ili hapo watakapofika Gibea ya Benyamini wapate kutenda mfano wa upumbavu huo wote walioutenda wao katika Israeli.

Nao wanaume wa Gibea wakaniondokea, na kuizingira hiyo nyumba pande zote juu yangu wakati wa usiku; walitaka kuniua, na suria wangu wakambaka nguvu, hata amekufa.

Basi nikamtwaa huyo suria wangu, na kumkata vipande, na kumpeleka katika nchi yote ya urithi wa Israeli; kwa sababu wametenda maovu makuu na upumbavu katika Israeli.

Ndipo Sauli akasema, Nimekosa; rudi, Daudi, mwanangu; maana sitakudhuru tena, kwa kuwa maisha yangu yalikuwa na thamani machoni pako leo; angalia, nimetenda upumbavu, nimekosa sana.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo