Ndipo nuru yako itakapopambazuka kama asubuhi, na uponyaji wako utatokea punde; na haki yako itakutangulia; utukufu wa BWANA utakufuata nyuma ukulinde.
Yoshua 6:9 - Swahili Revised Union Version Wale watu wenye silaha walikwenda mbele ya hao makuhani walioyapiga mabaragumu, na wale waliokuwa nyuma wakalifuata hilo sanduku; makuhani wakiyapiga mabaragumu walipokuwa wakienda. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wale watu wenye silaha wakawatangulia wale makuhani ambao walikuwa wanapiga mabaragumu, na walinzi wengine wakifuata nyuma ya sanduku hilo, huku mabaragumu yakilia kwa mfululizo. Biblia Habari Njema - BHND Wale watu wenye silaha wakawatangulia wale makuhani ambao walikuwa wanapiga mabaragumu, na walinzi wengine wakifuata nyuma ya sanduku hilo, huku mabaragumu yakilia kwa mfululizo. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wale watu wenye silaha wakawatangulia wale makuhani ambao walikuwa wanapiga mabaragumu, na walinzi wengine wakifuata nyuma ya sanduku hilo, huku mabaragumu yakilia kwa mfululizo. Neno: Bibilia Takatifu Walinzi waliokuwa na silaha wakaenda mbele ya hao makuhani waliopiga hizo baragumu na hao walinzi wa nyuma wakafuata Sanduku. Wakati wote huu baragumu zilikuwa zikipigwa. Neno: Maandiko Matakatifu Walinzi waliokuwa na silaha wakaenda mbele ya hao makuhani waliopiga hizo baragumu na hao walinzi wa nyuma wakafuata Sanduku. Wakati wote huu baragumu zilikuwa zikipigwa. BIBLIA KISWAHILI Wale watu wenye silaha walikwenda mbele ya hao makuhani waliopiga mabaragumu, na wale waliokuwa nyuma wakalifuata hilo sanduku; makuhani wakipiga mabaragumu walipokuwa wakienda. |
Ndipo nuru yako itakapopambazuka kama asubuhi, na uponyaji wako utatokea punde; na haki yako itakutangulia; utukufu wa BWANA utakufuata nyuma ukulinde.
Kisha beramu ya kambi ya wana wa Dani, ambayo ilikuwa ni nyuma ya makambi yote, ikasafiri, kwa majeshi yao; na juu ya jeshi lake ni Ahiezeri mwana wa Amishadai.
Yoshua akawaamuru watu, akasema Msipige kelele, wala sauti zenu zisisikiwe, wala neno lolote lisitoke kinywani mwenu, hadi siku ile nitakapowaamuru kupiga kelele, ndipo mtakapopiga kelele.
Na wale makuhani saba wakayachukua mabaragumu saba ya pembe za kondoo dume mbele ya sanduku la BWANA, wakaenda huku wakiyapiga mabaragumu; nao watu wenye silaha wakawatangulia, na hao waliokuwa nyuma wakalifuata sanduku la BWANA; huku makuhani wakiyapiga mabaragumu bila kukoma.
Basi ikawa Yoshua alipokwisha kusema na watu, wale makuhani saba, wenye kuzichukua baragumu saba za pembe za kondoo dume mbele za BWANA, watatangulia, wakayapiga hayo mabaragumu; nalo sanduku la Agano la BWANA likawafuata.