Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Isaya 58:8 - Swahili Revised Union Version

8 Ndipo nuru yako itakapopambazuka kama asubuhi, na uponyaji wako utatokea punde; na haki yako itakutangulia; utukufu wa BWANA utakufuata nyuma ukulinde.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

8 “Mkifanya hivyo mtangara kama pambazuko, mkiwa wagonjwa mtapona haraka. Matendo yenu mema yatawatangulia, nami nitawalindeni kutoka nyuma kwa utukufu wangu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

8 “Mkifanya hivyo mtangara kama pambazuko, mkiwa wagonjwa mtapona haraka. Matendo yenu mema yatawatangulia, nami nitawalindeni kutoka nyuma kwa utukufu wangu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

8 “Mkifanya hivyo mtang'ara kama pambazuko, mkiwa wagonjwa mtapona haraka. Matendo yenu mema yatawatangulia, nami nitawalindeni kutoka nyuma kwa utukufu wangu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

8 Ndipo nuru yako itajitokeza kama mapambazuko na uponyaji wako utatokea upesi; ndipo haki yako itakapokutangulia mbele yako, na utukufu wa Mwenyezi Mungu utakuwa mlinzi nyuma yako.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

8 Ndipo nuru yako itajitokeza kama mapambazuko na uponyaji wako utatokea upesi; ndipo haki yako itakapokutangulia mbele yako, na utukufu wa bwana utakuwa mlinzi nyuma yako.

Tazama sura Nakili




Isaya 58:8
27 Marejeleo ya Msalaba  

Na maisha yako yatakuwa meupe kuliko adhuhuri; Giza lake litakuwa kama alfajiri.


Nuru huwaangaza wenye adili gizani; Ana fadhili na huruma na haki.


Ataitokeza haki yako kama nuru, Na hukumu yako kama jina la adhuhuri.


Haki itakwenda mbele zake, Na kuzitayarishia hatua zake mapito.


Nuru humwangazia mwenye haki, Na furaha ni kwa wanyofu wa moyo.


Kisha malaika wa Mungu, aliyetangulia mbele ya jeshi la Israeli, akaondoka akaenda nyuma yao; na ile nguzo ya wingu ikaondoka hapo mbele yao, ikasimama nyuma yao;


Mwenye rehema huitendea mema nafsi yake; Aliye mkali hujisumbua mwili wake.


Nafsi ya mtu mkarimu itastawishwa; Anyweshaye atanyweshwa mwenyewe.


Bali njia ya wenye haki ni kama nuru ing'aayo, Ikizidi kung'aa hata mchana mkamilifu.


Fungueni malango yake, Taifa lenye haki, lishikalo kweli, liingie.


Na tena nuru ya mwezi itakuwa kama nuru ya jua, na nuru ya jua itaongezeka mara saba, kama nuru ya siku saba, katika siku ile BWANA atakapofunga mapigo ya watu wake, na kuliponya pigo la jeraha lao.


Wala hapana mwenyeji atakayesema, Mimi mgonjwa; watu wakaao humo watasamehewa uovu wao.


Maana hamtatoka kwa haraka, wala hamtakwenda kwa kukimbia, kwa sababu BWANA atawatangulia; na Mungu wa Israeli atawafuata nyuma; awalinde.


Nimeziona njia zake; nami nitamponya; nitamwongoza pia, nitamrudishia faraja zake, yeye na hao wanaomlilia.


Ondoka, uangaze; kwa kuwa nuru yako imekuja, Na utukufu wa BWANA umekuzukia.


Maana, tazama, giza litaifunika dunia, Na giza kuu litazifunika makabila ya watu; Bali BWANA atakuzukia wewe, Na utukufu wake utaonekana juu yako.


Kwa ajili ya Sayuni sitanyamaza, na kwa ajili ya Yerusalemu sitatulia, hata haki yake itakapotokea kama mwangaza, na wokovu wake kama taa iwakayo.


Maana nitakurudishia afya, nami nitakuponya majeraha yako, asema BWANA, kwa sababu wamekuita, mwenye kutupwa, wakisema, Ni Sayuni, mji ambao hakuna mtu autakaye.


Tazama, nitauletea afya na kupona, nami nitawaponya; nami nitawafunulia wingi wa amani na kweli.


Mimi nitawaponya kurudi nyuma kwao; nitawapenda kwa ukunjufu wa moyo; kwa maana hasira yangu imemwacha.


Lakini kwenu ninyi mnaolicha jina langu, jua la haki litawachomozea, likiwa na uwezo wa kuponya katika miale yake; nanyi mtatoka nje, na kuchezacheza kama ndama watokapo mazizini.


Maana mioyo ya watu hawa imekuwa mizito, Na kwa masikio yao hawasikii vema, Na macho yao wameyafumba; Wasije wakaona kwa macho yao, Wakasikia kwa masikio yao, Wakaelewa kwa mioyo yao, Wakaongoka, nikawaponya.


akasema, Kornelio, kuomba kwako kumesikiwa, na sadaka zako zinakumbukwa mbele za Mungu.


bali katika kila taifa mtu amchaye na kutenda haki hukubaliwa na yeye.


Akamkodolea macho, akaogopa akasema, Kuna nini, Bwana? Akamwambia, Sala zako na sadaka zako zimefika juu na kuwa ukumbusho mbele za Mungu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo