Yoshua 6:13 - Swahili Revised Union Version13 Na wale makuhani saba wakayachukua mabaragumu saba ya pembe za kondoo dume mbele ya sanduku la BWANA, wakaenda huku wakiyapiga mabaragumu; nao watu wenye silaha wakawatangulia, na hao waliokuwa nyuma wakalifuata sanduku la BWANA; huku makuhani wakiyapiga mabaragumu bila kukoma. Tazama suraMatoleo zaidiBiblia Habari Njema13 Wale makuhani saba wenye mabaragumu saba za kondoo dume walitembea mbele ya sanduku la Mwenyezi-Mungu wakipiga mabaragumu mfululizo. Watu wenye silaha walilitangulia sanduku la Mwenyezi-Mungu na walinzi wengine nyuma yake. Mabaragumu yakaendelea kupigwa. Tazama suraBiblia Habari Njema - BHND13 Wale makuhani saba wenye mabaragumu saba za kondoo dume walitembea mbele ya sanduku la Mwenyezi-Mungu wakipiga mabaragumu mfululizo. Watu wenye silaha walilitangulia sanduku la Mwenyezi-Mungu na walinzi wengine nyuma yake. Mabaragumu yakaendelea kupigwa. Tazama suraBiblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza13 Wale makuhani saba wenye mabaragumu saba za kondoo dume walitembea mbele ya sanduku la Mwenyezi-Mungu wakipiga mabaragumu mfululizo. Watu wenye silaha walilitangulia sanduku la Mwenyezi-Mungu na walinzi wengine nyuma yake. Mabaragumu yakaendelea kupigwa. Tazama suraNeno: Bibilia Takatifu13 Wale Makuhani saba waliobeba zile baragumu saba wakatangulia mbele ya Sanduku la Mwenyezi Mungu wakizipiga. Watu wenye silaha wakatangulia mbele yao na walinzi wa nyuma wakalifuata Sanduku la Mwenyezi Mungu, huku baragumu hizo zikiendelea kulia. Tazama suraNeno: Maandiko Matakatifu13 Wale Makuhani saba wakizibeba zile baragumu saba wakatangulia mbele ya Sanduku la bwana wakizipiga. Watu wenye silaha wakatangulia mbele yao na walinzi wa nyuma wakalifuata Sanduku la bwana, huku baragumu hizo zikiendelea kulia. Tazama suraBIBLIA KISWAHILI13 Na wale makuhani saba wakayachukua mabaragumu saba ya pembe za kondoo dume mbele ya sanduku la BWANA, wakaenda huku wakipiga mabaragumu; nao watu wenye silaha wakawatangulia, na hao waliokuwa nyuma wakalifuata sanduku la BWANA; huku makuhani wakipiga mabaragumu bila kukoma. Tazama sura |