Biblia ya mtandaoni

Matangazo

Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya

Yoshua 4:5 - Swahili Revised Union Version

naye Yoshua akawaambia, Haya, piteni ninyi mtangulie mbele ya sanduku la BWANA, Mungu wenu, mwende pale katikati ya Yordani, mkatwae kila mmoja wenu jiwe moja begani mwake, kwa kadiri ya hesabu ya makabila ya wana wa Israeli;

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

akawaambia, “Litangulieni sanduku la agano la Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, mpaka katikati ya mto Yordani. Kila mmoja wenu achukue jiwe begani mwake, jiwe moja kwa ajili ya kila kabila la Israeli.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

akawaambia, “Litangulieni sanduku la agano la Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, mpaka katikati ya mto Yordani. Kila mmoja wenu achukue jiwe begani mwake, jiwe moja kwa ajili ya kila kabila la Israeli.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

akawaambia, “Litangulieni sanduku la agano la Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, mpaka katikati ya mto Yordani. Kila mmoja wenu achukue jiwe begani mwake, jiwe moja kwa ajili ya kila kabila la Israeli.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

naye akawaambia, “Mtangulie mbele ya Sanduku la Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, mwende katikati ya Mto Yordani. Kila mmoja wenu atainua jiwe begani mwake, kulingana na idadi ya makabila ya Israeli,

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

naye akawaambia, “Mtangulie mbele ya Sanduku la bwana Mwenyezi Mungu wenu, mwende katikati ya Mto Yordani. Kila mmoja wenu atainua jiwe begani mwake, kufuatana na hesabu ya makabila ya Waisraeli,

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

naye Yoshua akawaambia, Haya, piteni ninyi mtangulie mbele ya sanduku la BWANA, Mungu wenu, mwende pale katikati ya Yordani, mkatwae kila mmoja wenu jiwe moja begani mwake, kwa kadiri ya hesabu ya makabila ya wana wa Israeli;

Tazama sura
Tafsiri zingine

Yoshua 4:5
7 Marejeleo ya Msalaba  

Yakobo akawaambia ndugu zake, Kusanyeni mawe. Wakatwaa mawe, wakafanya chungu, nao wakala huko karibu na ile chungu.

Basi Musa akayaandika maneno yote ya BWANA, akaondoka asubuhi na mapema, akajenga madhabahu chini ya mlima, na nguzo kumi na mbili, kwa hesabu ya makabila kumi na mawili ya Israeli,

Na iwe, siku mtakayovuka Yordani kwenda nchi akupayo BWANA, Mungu wako, ujisimamishie mawe makubwa, ukayatalize matalizo,

Sikiza, Ee Israeli; hivi leo unataka kuvuka Yordani uingie kwa kuwamiliki mataifa yaliyo makubwa, na yenye nguvu kukupita, miji mikubwa iliyojengewa kuta hadi mbinguni,

Nao walipofika pande za Yordani zilizo katika nchi ya Kanaani, hao wana wa Reubeni, na wana wa Gadi, na nusu ya kabila la Manase, wakajenga madhabahu huko karibu na Yordani, iliyoonekana kuwa ni madhabahu kubwa.

Basi Yoshua akawaita hao watu kumi na wawili, aliokuwa ameteua tangu hapo awali, katika wana wa Israeli, kila kabila mtu mmoja;

ili kwamba jambo hili liwe ishara kati yenu, hapo watoto wenu watakapowauliza ninyi katika siku zijazo, wakisema, Ni nini maana yake mawe haya?