Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Kutoka 24:4 - Swahili Revised Union Version

4 Basi Musa akayaandika maneno yote ya BWANA, akaondoka asubuhi na mapema, akajenga madhabahu chini ya mlima, na nguzo kumi na mbili, kwa hesabu ya makabila kumi na mawili ya Israeli,

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 Mose akayaandika maagizo yote ambayo Mwenyezi-Mungu alimpa. Kisha akaamka asubuhi na mapema, akajenga madhabahu chini ya mlima na kusimamisha nguzo kumi na mbili kulingana na idadi ya makabila kumi na mbili ya Israeli.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 Mose akayaandika maagizo yote ambayo Mwenyezi-Mungu alimpa. Kisha akaamka asubuhi na mapema, akajenga madhabahu chini ya mlima na kusimamisha nguzo kumi na mbili kulingana na idadi ya makabila kumi na mbili ya Israeli.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 Mose akayaandika maagizo yote ambayo Mwenyezi-Mungu alimpa. Kisha akaamka asubuhi na mapema, akajenga madhabahu chini ya mlima na kusimamisha nguzo kumi na mbili kulingana na idadi ya makabila kumi na mbili ya Israeli.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 Ndipo Musa akaandika kila kitu Mwenyezi Mungu alichokuwa amesema. Akaamka kesho yake asubuhi na mapema na kujenga madhabahu chini ya mlima na kusimamisha nguzo kumi na mbili za mawe kuwakilisha makabila kumi na mawili ya Israeli.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 Ndipo Musa akaandika kila kitu bwana alichokuwa amesema. Akaamka kesho yake asubuhi na mapema na kujenga madhabahu chini ya mlima na kusimamisha nguzo kumi na mbili za mawe kuwakilisha makabila kumi na mawili ya Israeli.

Tazama sura Nakili




Kutoka 24:4
27 Marejeleo ya Msalaba  

BWANA akamtokea Abramu, akasema, Uzao wako nitawapa nchi hii. Naye akamjengea BWANA madhabahu huko alikomtokea.


Yakobo akaondoka asubuhi na mapema, akalitwaa lile jiwe aliloliweka chini ya kichwa chake, akalisimamisha kama nguzo, na kumimina mafuta juu yake.


Na jiwe hili nililosimamisha kama nguzo litakuwa nyumba ya Mungu; na katika kila utakalonipa hakika nitakutolea wewe sehemu ya kumi.


Yakobo akatwaa jiwe akalisimamisha kama nguzo.


Ahiya akalishika lile vazi jipya alilokuwa amelivaa, akalirarua vipande kumi na viwili.


Eliya akatwaa mawe kumi na mawili, kwa hesabu ya makabila ya wana wa Yakobo, aliyejiliwa na neno la BWANA na kuambiwa, Jina lako litakuwa Israeli.


Na katika kuiweka wakfu nyumba ya Mungu, wakatoa sadaka, ng'ombe mia moja, na kondoo dume mia mbili, na wana-kondoo mia nne; tena wakatoa mbuzi dume kumi na wawili, kuwa sadaka ya dhambi kwa ajili ya Waisraeli wote, kwa hesabu ya makabila ya Israeli.


Basi hawa ndio waliotia mhuri; Nehemia, ndiye Tirshatha, mwana wa Hakalia, na Sedekia;


BWANA akamwambia Musa, Andika habari hii katika kitabu iwe ukumbusho, kisha ihubiri masikioni mwa Yoshua; ya kuwa nitaufuta ukumbusho wa Amaleki kabisa, usiwe tena chini ya mbingu.


Musa akajenga madhabahu, akaiita jina lake Yahweh-nisi;


Basi hukumu utakazoziweka mbele ya watu ni hizi


Kisha akakitwaa Kitabu cha Agano akakisoma masikioni mwa watu; wakasema, Hayo yote aliyoyanena BWANA tutayatenda, nasi tutatii.


Na vile vito vitakuwa sawasawa na majina ya wana wa Israeli, kumi na viwili, sawasawa na majina yao; mfano wa kuchora kwa mihuri kila kimoja sawasawa na jina lake, vitakuwa vya hayo makabila kumi na mawili.


BWANA akamwambia Musa, Andika maneno haya; kwa kuwa mimi nimefanya agano nawe, na pamoja na Israeli, kwa mujibu wa maneno haya.


Katika siku hiyo itakuwako madhabahu katika nchi ya Misri kwa BWANA, na nguzo mpakani mwake kwa BWANA.


Nawe utatwaa unga mwembamba, na kuoka mikate kumi na miwili ya huo unga; sehemu za kumi mbili za efa, zitakuwa katika mkate mmoja.


Nena na wana wa Israeli, kisha upokee kwao fimbo, fimbo moja kwa ajili ya nyumba ya kila baba, katika wakuu wao wote, kama nyumba za baba zao zilivyo, fimbo kumi na mbili; kisha andika jina la kila mtu katika fimbo yake.


mpate kula na kunywa mezani pangu katika ufalme wangu; na kuketi katika viti vya enzi, huku mkiyahukumu makabila kumi na mawili ya Israeli.


tena Yakobo, Kefa, na Yohana, waliosifika kuwa ni nguzo, walipoitambua ile neema niliyopewa, walinipa mimi na Barnaba mkono wa kulia wa kuonesha ushirikiano; ili sisi tuende kwa Mataifa, na wao waende kwa watu wa tohara;


Musa akaiandika torati hii, akawapa makuhani, wana wa Lawi, waliolichukua sanduku la Agano la BWANA, na wazee wote wa Israeli.


Na yale mawe kumi na mawili waliyoyatwaa katikati ya Yordani Yoshua akayasimamisha Gilgali.


naye Yoshua akawaambia, Haya, piteni ninyi mtangulie mbele ya sanduku la BWANA, Mungu wenu, mwende pale katikati ya Yordani, mkatwae kila mmoja wenu jiwe moja begani mwake, kwa kadiri ya hesabu ya makabila ya wana wa Israeli;


Na ukuta wa mji ulikuwa na misingi kumi na miwili, na katika ile misingi kulikuwa na majina kumi na mawili ya wale mitume kumi na wawili wa Mwana-kondoo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo