Wana wa Zilpa, kijakazi wa Lea, ni Gadi na Asheri. Hawa ndio wana wa Yakobo aliozaliwa katika Padan-aramu.
Yoshua 19:24 - Swahili Revised Union Version Kisha sehemu ya tano ilitokea kwa ajili ya kabila la wana wa Asheri kwa kufuata jamaa zao. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kura ya tano ilizipata koo za kabila la Asheri. Biblia Habari Njema - BHND Kura ya tano ilizipata koo za kabila la Asheri. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kura ya tano ilizipata koo za kabila la Asheri. Neno: Bibilia Takatifu Kura ya tano ikaangukia kabila la Asheri, kufuatana na koo zao. Neno: Maandiko Matakatifu Kura ya tano ikaangukia kabila la Asheri, ukoo kwa ukoo. BIBLIA KISWAHILI Kisha sehemu ya tano ilitokea kwa ajili ya kabila la wana wa Asheri kwa kufuata jamaa zao. |
Wana wa Zilpa, kijakazi wa Lea, ni Gadi na Asheri. Hawa ndio wana wa Yakobo aliozaliwa katika Padan-aramu.
Tena mpakani mwake Dani, toka upande wa mashariki hadi upande wa magharibi; Asheri, fungu moja.
Huu ndio urithi wa kabila la wana wa Isakari kwa kufuata jamaa zao; miji hiyo pamoja na vijiji vyake.
Asheri naye hakuwatoa wenyeji wa Aka, wala hao waliokaa Sidoni, wala hao wa Alabu, wala hao wa Akzibu, wala hao wa Helba, wala hao wa Afeka, wala hao wa Rehobu;
Gileadi alikaa ng'ambo ya Yordani, Na Dani, mbona alikaa katika merikebu? Asheri alikaa kimya penye bandari ya bahari, Alikaa katika hori zake.