kisha ikateremkia upande wa magharibi hadi kuufikia mpaka wa Wayafleti, hadi mpaka wa Beth-horoni ya chini, hadi kufikia Gezeri; na matokeo yake yalikuwa hapo baharini.
Yoshua 17:9 - Swahili Revised Union Version Tena mpaka uliteremka hadi kijito cha Kana, upande wa kusini wa hicho kijito; miji hiyo ilikuwa ya Efraimu kati ya miji ya Manase; na mpaka wa Manase ulikuwa upande wa kaskazini wa hicho kijito, na mwisho wake ulikuwa baharini; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mpaka huo uliendelea hadi kijito cha Kana. Miji iliyokuwa kusini ya Kana ilikuwa ya Waefraimu hata ingawa ilikuwa katika nchi ya kabila la Manase. Halafu mpaka ukapita kaskazini ya kijito Kana na kuishia bahari ya Mediteranea. Biblia Habari Njema - BHND Mpaka huo uliendelea hadi kijito cha Kana. Miji iliyokuwa kusini ya Kana ilikuwa ya Waefraimu hata ingawa ilikuwa katika nchi ya kabila la Manase. Halafu mpaka ukapita kaskazini ya kijito Kana na kuishia bahari ya Mediteranea. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mpaka huo uliendelea hadi kijito cha Kana. Miji iliyokuwa kusini ya Kana ilikuwa ya Waefraimu hata ingawa ilikuwa katika nchi ya kabila la Manase. Halafu mpaka ukapita kaskazini ya kijito Kana na kuishia bahari ya Mediteranea. Neno: Bibilia Takatifu Kisha mpaka ule uliendelea kuelekea kusini hadi Bonde la Kana. Kulikuwa na miji ya Efraimu iliyokuwa miongoni mwa miji ya Manase, lakini mpaka wa Manase ulikuwa upande wa kaskazini wa lile bonde, na kuishia kwenye bahari. Neno: Maandiko Matakatifu Kisha mpaka ule uliendelea kuelekea kusini hadi Bonde la Kana. Kulikuwepo miji ya Efraimu iliyokuwa miongoni mwa miji ya Manase, lakini mpaka wa Manase ulikuwa upande wa kaskazini wa lile bonde na kuishia kwenye bahari. BIBLIA KISWAHILI Tena mpaka uliteremka hadi kijito cha Kana, upande wa kusini wa hicho kijito; miji hiyo ilikuwa ya Efraimu kati ya miji ya Manase; na mpaka wa Manase ulikuwa upande wa kaskazini wa hicho kijito, na mwisho wake ulikuwa baharini; |
kisha ikateremkia upande wa magharibi hadi kuufikia mpaka wa Wayafleti, hadi mpaka wa Beth-horoni ya chini, hadi kufikia Gezeri; na matokeo yake yalikuwa hapo baharini.
upande wa kusini ilikuwa ni mali ya Efraimu, na upande wa kaskazini ilikuwa ni mali ya Manase, na bahari ilikuwa mpaka wake; nao wakafika hadi Asheri upande wa kaskazini, na kufika hata Isakari upande wa mashariki.
kisha mpaka ulizunguka kuelekea Rama, na mji wa Tiro ulio na boma; kisha mpaka ulizunguka kuelekea Hosa; na matokeo yake yalikuwa baharini katika nchi ya Akzibu;