na Ishmaya Mgibeoni, shujaa wa wale thelathini, naye alikuwa juu ya wale thelathini; na Yeremia, na Yahazieli, na Yohana, na Yozabadi Mgederathi;
Yoshua 15:36 - Swahili Revised Union Version Shaarimu, Adithaimu, Gedera na Gederothaimu miji kumi na minne, pamoja na vijiji vyake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Shaaraimu, Adithaimu, Gedera na Gederothaimu. Jumla ya miji waliyopewa ni kumi na minne pamoja na vijiji vyake. Biblia Habari Njema - BHND Shaaraimu, Adithaimu, Gedera na Gederothaimu. Jumla ya miji waliyopewa ni kumi na minne pamoja na vijiji vyake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Shaaraimu, Adithaimu, Gedera na Gederothaimu. Jumla ya miji waliyopewa ni kumi na minne pamoja na vijiji vyake. Neno: Bibilia Takatifu Shaaraimu, Adithaimu na Gedera (au Gederothaimu); yote ni miji kumi na nne, pamoja na vijiji vyake. Neno: Maandiko Matakatifu Shaaraimu, Adithaimu na Gedera (au Gederothaimu); yote ni miji kumi na minne, pamoja na vijiji vyake. BIBLIA KISWAHILI Shaarimu, Adithaimu, Gedera na Gederothaimu miji kumi na minne, pamoja na vijiji vyake. |
na Ishmaya Mgibeoni, shujaa wa wale thelathini, naye alikuwa juu ya wale thelathini; na Yeremia, na Yahazieli, na Yohana, na Yozabadi Mgederathi;
na juu ya mizeituni na mikuyu iliyokuwamo katika Shefela alikuwa Baal-hanani, Mgederi; na juu ya ghala za mafuta alikuwa Yoashi;
Nao watu wa Israeli na wa Yuda wakainuka, na kupiga kelele, nao wakawafuata Wafilisti mpaka Gathi, na mpaka malango ya Ekroni. Nao majeruhi wa Wafilisti wakaanguka kando ya njia iendayo Shaarimu, mpaka Gathi, na mpaka Ekroni.