Na wana wa Gershoni wakapewa, katika jamaa ya nusu kabila ya Manase; Golani katika Bashani pamoja na viunga vyake, na Ashtarothi pamoja na viunga vyake;
Yoshua 13:31 - Swahili Revised Union Version na nusu ya Gileadi, na Ashtarothi, na Edrei, hiyo miji ya ufalme wa Ogu katika Bashani, ilikuwa ni ya wana wa Makiri mwana wa Manase maana, kwa hiyo nusu ya wana wa Makiri sawasawa na jamaa zao. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema nusu ya Gileadi, Ashtarothi, Edrei, ambayo ilikuwa chini ya himaya ya mfalme Ogu wa Bashani; Eneo hili walipewa nusu ya wazawa wa Makiri mwana wa Manase, kulingana na koo zao. Biblia Habari Njema - BHND nusu ya Gileadi, Ashtarothi, Edrei, ambayo ilikuwa chini ya himaya ya mfalme Ogu wa Bashani; Eneo hili walipewa nusu ya wazawa wa Makiri mwana wa Manase, kulingana na koo zao. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza nusu ya Gileadi, Ashtarothi, Edrei, ambayo ilikuwa chini ya himaya ya mfalme Ogu wa Bashani; Eneo hili walipewa nusu ya wazawa wa Makiri mwana wa Manase, kulingana na koo zao. Neno: Bibilia Takatifu nusu ya Gileadi, na Ashtarothi na Edrei (miji ya kifalme ya Ogu katika Bashani). Hii ilikuwa kwa ajili ya wazao wa Makiri mwana wa Manase, kwa ajili ya nusu ya wana wa Makiri, kufuatana na koo zao. Neno: Maandiko Matakatifu nusu ya Gileadi, na Ashtarothi na Edrei (miji ya kifalme ya Ogu katika Bashani). Hii ilikuwa kwa ajili ya wazao wa Makiri mwana wa Manase, kwa ajili ya nusu ya wana wa Makiri, ukoo kwa ukoo. BIBLIA KISWAHILI na nusu ya Gileadi, na Ashtarothi, na Edrei, hiyo miji ya ufalme wa Ogu katika Bashani, ilikuwa ni ya wana wa Makiri mwana wa Manase, kwa hiyo nusu ya wana wa Makiri sawasawa na jamaa zao. |
Na wana wa Gershoni wakapewa, katika jamaa ya nusu kabila ya Manase; Golani katika Bashani pamoja na viunga vyake, na Ashtarothi pamoja na viunga vyake;
Gileadi ni yangu, na Manase ni yangu, Na Efraimu ni kinga ya kichwa changu. Yuda ni fimbo yangu ya kifalme,
Na mpakani mwa Naftali, toka upande wa mashariki hadi upande wa magharibi; Manase, fungu moja.
tena mpaka wa Ogu mfalme wa Bashani, aliyekuwa wa hayo mabaki ya hao Warefai, aliyekaa Ashtarothi na Edrei,
ufalme wote wa Ogu uliokuwa katika Bashani, huyo aliyekuwa akitawala katika Ashtarothi na katika Edrei (huyo alisalia katika mabaki ya wale Warefai); kwa kuwa Musa aliwapiga hao na kuwafukuza.
Hizi ndizo mirathi ambazo Musa alizigawanya katika nchi tambarare za Moabu, ng'ambo ya pili ya Yordani, kukabili Yeriko, upande wa mashariki.
Kisha kura zilizomwangukia Manase zilikuwa ni sehemu kumi, mbali na nchi ya Gileadi na Bashani, iliyo ng'ambo ya Yordani;
kwa sababu hao binti za Manase walikuwa na urithi katika wanawe wa kiume; na nchi ya Gileadi ilikuwa ni mali ya hao wana wa kiume wa Manase waliosalia.
na habari ya hayo yote aliyowatenda wale wafalme wawili wa Waamori, waliokuwa huko ng'ambo ya pili ya Yordani, maana huyo Sihoni, mfalme wa Heshboni, na Ogu, mfalme wa Bashani, aliyekuwa huko Ashtarothi.
Kisha wana wa Israeli walifanya tena yaliyo maovu mbele za macho ya BWANA, wakawatumikia Mabaali, na Maashtorethi, na miungu ya Shamu, na miungu ya Sidoni, na miungu ya Moabu, na miungu ya wana wa Amoni, na miungu ya Wafilisti; nao wakamuacha BWANA, wala hawakumtumikia yeye.
Gileadi alikaa ng'ambo ya Yordani, Na Dani, mbona alikaa katika merikebu? Asheri alikaa kimya penye bandari ya bahari, Alikaa katika hori zake.
Nao wakamlilia BWANA, wakasema, Tumefanya dhambi, kwa kuwa tumemwacha BWANA, na kuwatumikia Mabaali na Maashtorethi; lakini sasa tuokoe kutoka kwa mikono ya adui zetu, nasi tutakutumikia wewe.
Basi Samweli akawaambia nyumba yote ya Israeli, akasema, Ikiwa mnamrudia BWANA kwa mioyo yenu yote, basi, iondoleeni mbali miungu migeni, nayo Maashtorethi yatoke kwenu, mkamwelekezee BWANA mioyo yenu, mkamtumikie yeye peke yake; naye atawaokoa katika mikono ya Wafilisti.