Wana wa Lea ni Reubeni, mzaliwa wa kwanza wa Yakobo, na Simeoni, na Lawi, na Yuda, na Isakari, na Zabuloni.
Yoshua 13:15 - Swahili Revised Union Version Musa akawapa kabila la wana wa Reubeni kwa kadiri ya jamaa zao. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Sehemu ya nchi ambayo Mose aliwapa watu wa kabila la Reubeni kulingana na jamaa zao, Biblia Habari Njema - BHND Sehemu ya nchi ambayo Mose aliwapa watu wa kabila la Reubeni kulingana na jamaa zao, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Sehemu ya nchi ambayo Mose aliwapa watu wa kabila la Reubeni kulingana na jamaa zao, Neno: Bibilia Takatifu Haya ndio maeneo ambayo Musa alikuwa amewapa kabila la Reubeni kufuatana na koo zao: Neno: Maandiko Matakatifu Haya ndiyo maeneo ambayo Musa alikuwa amewapa kabila la Reubeni ukoo kwa ukoo: BIBLIA KISWAHILI Musa akawapa kabila la wana wa Reubeni kwa kadiri ya jamaa zao. |
Wana wa Lea ni Reubeni, mzaliwa wa kwanza wa Yakobo, na Simeoni, na Lawi, na Yuda, na Isakari, na Zabuloni.
Hawa ndio vichwa vya nyumba za baba zao: wana wa Reubeni, mzaliwa wa kwanza wa Israeli; ni Hanoki, na Palu, na Hesroni, na Karmi; hao ni jamaa za Reubeni.
Na mpakani mwa Efraimu, toka upande wa mashariki hadi upande wa magharibi; Reubeni, fungu moja.
Lakini hakuwapa watu wa kabila la Lawi urithi wowote ule; maana sadaka za BWANA, Mungu wa Israeli, zisongezwazo kwa njia ya moto ndizo urithi wake huyo, kama alivyomwambia.
Mpaka wao ulikuwa kutoka hapo Aroeri, iliyo pale ukingoni mwa bonde la Arnoni, na huo mji ulio katikati ya bonde, na nchi tambarare yote iliyo karibu na Medeba;
Na sasa yeye BWANA, Mungu wenu, amewapa ndugu zenu kustarehe, kama alivyowaambia; basi sasa rudini ninyi mwende mahemani kwenu, hata nchi ya milki yenu, ambayo huyo Musa, mtumishi wa BWANA, aliwapa ng'ambo ya pili ya Yordani.
Lakini huyo Sihoni hakuwaamini Israeli ili wapite ndani ya mpaka wake; bali Sihoni akawakutanisha watu wake wote, nao wakapiga kambi katika Yahasa, wakapigana na Israeli.