Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Yoshua 13:14 - Swahili Revised Union Version

14 Lakini hakuwapa watu wa kabila la Lawi urithi wowote ule; maana sadaka za BWANA, Mungu wa Israeli, zisongezwazo kwa njia ya moto ndizo urithi wake huyo, kama alivyomwambia.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 Mose hakuwapa watu wa kabila la Lawi nchi yoyote. Bali tambiko walizomtolea Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli kwa moto, hizo ndizo zilizokuwa fungu lao, kama Mwenyezi-Mungu alivyomwambia Mose.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

14 Mose hakuwapa watu wa kabila la Lawi nchi yoyote. Bali tambiko walizomtolea Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli kwa moto, hizo ndizo zilizokuwa fungu lao, kama Mwenyezi-Mungu alivyomwambia Mose.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 Mose hakuwapa watu wa kabila la Lawi nchi yoyote. Bali tambiko walizomtolea Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli kwa moto, hizo ndizo zilizokuwa fungu lao, kama Mwenyezi-Mungu alivyomwambia Mose.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 Lakini kwa kabila la Lawi, Musa hakupeana urithi, kwa kuwa sadaka za kuteketezwa kwa moto zilizotolewa kwa Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, ndizo zilikuwa urithi wao, kama alivyowaahidi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 Lakini kwa kabila la Lawi, Musa hakupeana urithi, kwa kuwa sadaka za kuteketezwa kwa moto zilizotolewa kwa bwana, Mungu wa Israeli, ndizo zilizokuwa urithi wao, kama alivyowaahidi.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

14 Lakini hakuwapa watu wa kabila la Lawi urithi wowote ule; maana sadaka za BWANA, Mungu wa Israeli, zisongezwazo kwa njia ya moto ndizo urithi wake huyo, kama alivyomwambia.

Tazama sura Nakili

Yoshua 13:14
12 Marejeleo ya Msalaba  

Nao watakuwa na urithi; mimi ni urithi wao; wala hamtawapa milki iwayo yote katika Israeli; mimi ni milki yao.

Wataila sadaka ya unga, na sadaka ya dhambi, na sadaka ya hatia, na kila kitu katika Israeli kilichowekwa wakfu kitakuwa chao.

Ndipo asiwe na fungu Lawi, wala urithi pamoja na nduguze; BWANA ndiye urithi wake, kwa mfano wa vile alivyomwambia BWANA, Mungu wako.)

Nanyi mtafurahi mbele za BWANA, Mungu wenu, ninyi, na wana wenu, na binti zenu, na watumishi wenu wa kiume na wa kike, na Mlawi aliyemo malangoni mwenu; kwa kuwa hana sehemu wala urithi kwenu.

Jilinde nafsi yako usimpuuze Mlawi siku zote utakazoishi katika nchi yako.

Pamoja na hayo wana wa Israeli hawakuwafukuza Wageshuri, wala Wamaaka; lakini Wageshuri na Wamaaka wamekaa kati ya Israeli, hadi siku hii ya leo.

Musa akawapa kabila la wana wa Reubeni kwa kadiri ya jamaa zao.

Lakini Musa hakuwapa kabila la Lawi urithi uwao wote; yeye BWANA, Mungu wa Israeli, ndiye urithi wao, kama alivyowaambia.

Kwa maana Walawi hawana fungu kati yenu; Kwa kuwa huo ukuhani wa BWANA ndio urithi wao; tena Gadi, na Reubeni, na hiyo nusu ya kabila la Manase, wamekwisha pata urithi wao ng'ambo ya pili ya Yordani upande wa mashariki, ambao walipewa na Musa, mtumishi wa BWANA.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo