Yoshua 10:38 - Swahili Revised Union Version Kisha Yoshua akarudi, na Israeli wote pamoja naye, hata Debiri; nao wakapigana nao; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kisha, Yoshua na Waisraeli wote wakarudi Debiri, wakaushambulia. Biblia Habari Njema - BHND Kisha, Yoshua na Waisraeli wote wakarudi Debiri, wakaushambulia. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kisha, Yoshua na Waisraeli wote wakarudi Debiri, wakaushambulia. Neno: Bibilia Takatifu Ndipo Yoshua na Waisraeli wote wakageuka na kushambulia Debiri. Neno: Maandiko Matakatifu Ndipo Yoshua na Israeli wote wakageuka na kuushambulia Debiri. BIBLIA KISWAHILI Kisha Yoshua akarudi, na Israeli wote pamoja naye, hata Debiri; nao wakapigana nao; |
wakautwaa, na kuupiga kwa makali ya upanga, na mfalme wake, na miji yake yote, na wote waliokuwamo ndani yake; hakumwacha aliyesalia hata mtu mmoja, sawasawa na hayo yote aliyoufanyia huo mji wa Egloni; lakini akauangamiza kabisa, na wote pia waliokuwamo ndani yake.
kisha akautwaa, na mfalme wake, na miji yake yote; nao wakawapiga kwa makali ya upanga, wakawaangamiza kabisa wote pia waliokuwamo ndani yake; hakumwacha hata mmoja aliyesalia; kama alivyoufanyia Hebroni aliufanyia na Debiri vivyo hivyo, na mfalme wake; kama alivyoufanyia Libna, na mfalme wake.
Kisha akakwea kutoka huko ili kuwaendea wenyeji wa Debiri; jina la Debiri hapo kwanza lilikuwa Kiriath-seferi.