lakini Mungu akawazungusha hao watu kwa njia ya bara kando ya Bahari ya Shamu; wana wa Israeli wakakwea kutoka nchi ya Misri wakiwa tayari kwa vita.
Yoshua 1:14 - Swahili Revised Union Version Wake zenu, na watoto wenu, na makundi yenu, watakaa katika nchi aliyowapa Musa ng'ambo ya Yordani; bali ninyi mtawatangulia ndugu zenu kuvuka, mkiwa mmevaa silaha zenu, watu wote wenye nguvu, na ushujaa, ili mpate kuwasaidia; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wake zenu, watoto wenu na wanyama wenu wa kufugwa watabaki katika nchi hiyo ambayo Mose aliwapeni, ngambo ya mto Yordani. Lakini wanaume wote hodari wakiwa na silaha watavuka mto na kuwatangulia ndugu zenu. Biblia Habari Njema - BHND Wake zenu, watoto wenu na wanyama wenu wa kufugwa watabaki katika nchi hiyo ambayo Mose aliwapeni, ngambo ya mto Yordani. Lakini wanaume wote hodari wakiwa na silaha watavuka mto na kuwatangulia ndugu zenu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wake zenu, watoto wenu na wanyama wenu wa kufugwa watabaki katika nchi hiyo ambayo Mose aliwapeni, ng'ambo ya mto Yordani. Lakini wanaume wote hodari wakiwa na silaha watavuka mto na kuwatangulia ndugu zenu. Neno: Bibilia Takatifu Wake zenu, watoto wenu na mifugo yenu watakaa katika nchi ambayo Musa aliwapa mashariki mwa Yordani, lakini wapiganaji wenu wote, wakiwa wamejiandaa kwa vita, lazima wavuke mbele ya ndugu zenu. Imewapasa kuwasaidia ndugu zenu, Neno: Maandiko Matakatifu Wake zenu, watoto wenu na mifugo yenu watakaa katika nchi ile Musa aliyowapa mashariki ya Yordani, lakini mashujaa wenu wote, wakiwa wamevikwa silaha kikamilifu lazima wavuke mbele ya ndugu zenu. Imewapasa kuwasaidia ndugu zenu hadi BIBLIA KISWAHILI Wake zenu, na watoto wenu, na makundi yenu, watakaa katika nchi aliyowapa Musa ng'ambo ya Yordani; bali ninyi mtawatangulia ndugu zenu kuvuka, mkiwa mmevaa silaha zenu, watu wote wenye nguvu, na ushujaa, ili mpate kuwasaidia; |
lakini Mungu akawazungusha hao watu kwa njia ya bara kando ya Bahari ya Shamu; wana wa Israeli wakakwea kutoka nchi ya Misri wakiwa tayari kwa vita.
Watoto wetu, na wake wetu, na kondoo wetu, na ng'ombe wetu wote, watakuwa hapo katika miji ya Gileadi;
Tena maofisa na waseme zaidi na watu, wawaambie, Ni mtu gani aliye hapa tena mwenye hofu na moyo mnyonge? Aende akarudi nyumbani kwake, isije mioyo ya nduguze ikayeyuka mfano wa moyo wake.
Lakini wake wenu na watoto wenu, na wanyama wenu wa mji, (nawajua kwamba mna wanyama wengi), na wakae katika miji yenu niliyowapa;
Akajichagulia sehemu ya kwanza, Kwani ndiko lilikowekwa fungu la mtoa-sheria; Akaja pamoja na wakuu wa watu, Akaitekeleza haki ya BWANA, Na hukumu zake kwa Israeli.
Likumbukeni neno lile alilowaamuru Musa mtumishi wa BWANA, akisema, BWANA, Mungu wenu, anawapa ninyi raha, naye atawapa nchi hii.
hadi BWANA atakapowapa ndugu zenu raha, kama alivyowapa ninyi, na wao pia wamepata kuimiliki nchi awapayo BWANA, Mungu wenu; ndipo mtakapoirudia nchi ya milki yenu na kuimiliki, ambayo Musa mtumishi wa BWANA aliwapeni ng'ambo ya Yordani upande wa maawio ya jua.
Na wana wa Reubeni, na wana wa Gadi na hiyo nusu ya kabila la Manase, wakavuka, wakiwa wamebeba silaha mbele ya wana wa Israeli, kama Musa alivyowaambia;
Na mwanamke yule alikuwa amevikwa nguo ya rangi ya zambarau, na nyekundu, amepambwa kwa dhahabu, na kito cha thamani, na lulu, naye alikuwa na kikombe cha dhahabu mkononi mwake, kilichojawa na machukizo, na machafu ya uasherati wake.